Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pacman usimchezee kabisa

Muktasari:

Alipotangaza kustaafu sambamba na mwenzake Floyd Mayweather ulingo wa ndondi ulipungua msisimko, ila Pacman aliurejesha na kuonyesha mojawapo ya mapambano yake bora.

        WIKIE NDI iliyo pita bondia mkongwe Manny ‘Pacman’ Pacquiao aliyetangaza kustaafu ngumi Aprili mwaka huu, alikatiza safari yake ya kustaafu na kurejea ulingoni kwa kishindo, akamchapa Jersie Vargas kisha akatwaa taji la WBO Welterweight kwa mara ya tatu.

Alipotangaza kustaafu sambamba na mwenzake Floyd Mayweather ulingo wa ndondi ulipungua msisimko, ila Pacman aliurejesha na kuonyesha mojawapo ya mapambano yake bora.

Pamoja na uzee wake katika fani, akiwa na umri wa miaka 37, Pacman alikuwa katika ubora wake alipomdunda mpinzani mchanga vargas 27, kwa pointi 114-113, 118-109 na 118-109.

Pambano hilo lilikuwa la kihistoria kwa kuwa wadau wengi walitilia shaka uwezo wa Pacquiao kufanya maangamizi kutokana na kuhisi kachuja.

Ila dhidi ya Vargas, Manny aliwaacha mashabiki vinywa wazi kwa mzigo alioupiga katika Ukumbi wa Thomas and Mack Center, Las Vegas .

Hili limesababisha Mwanaspoti kuchambua mapambano matano bomba kati ya 66 aliyopigana katika kipindi chote cha kupigana kwake.

Manny v Miguel Cotto

Ukumbi: MGM Grand, Las Vegas (Nov. 2009)

Taji: WBO Welterweight

Alikutana na Cotto kutoka Puerto Rico katika pambano lililoitwa Firepower. Cotto alikuwa akiogopewa sana kwa sababu alikuwa kapoteza mara moja tu katika maisha yake ya ngumi. Wengi waliamini kuwa angempa kibarua cha uhakika Manny. Cotto alianza vizuri raundi ya kwanza lakini kasi ya makonde mengi ya mfululizo kutoka kwa Manny yalimzidia na kumlewesha katika raundi ya tatu na nne, zote akilambishwa sakafu. Toka hapo ikawa tatizo kwa Cotto kumbana Manny.

Kufikia raundi ya 12, uso wa Cotto ulikuwa ni manundu matupu huku akitapakaa damu kote. Kwa kuogopa hali yake, mwamuzi Kenny Bayles alikatisha pambano hilo na Manny akatawazwa bingwa.

Manny v Oscar Del Hoya

Ukumbi: MGM Grand, Las Vegas (Des. 2008)

Taji: Hakuna

Pambano hili lililokwenda kwa jina la ‘Dream Match’ ndilo lililosababisha Golden Boy, Del Hoya kustaafu ngumi kabisa na kuwa promota. Del Hoya alibatizwa jina Golden boy kutokana na staili yake ya vita na alikuwa mzuri kujilinda na angemaliza pambano bila ya kuchafuliwa sura, ila mbele ya Manny kilitokea kituko. Katika pambano hilo lililokwenda kwa jina la ‘Dream Match’ Del Hoya alianza kwa kasi kubwa na umakini kitu kilichomtia uoga Manny. Lakini kasi ya ngumi za Manny zilimchanganya na kufikia raundi ya tano, jicho lake la kushoto lilikuwa likielekea kuziba. Kwenye raundi ya nane, timu yake Del hoya ilimwomba refa amalize pambano na ikawa ndiyo mwisho wa kupigana masumbwi.

Manny v Manuel Marquez II

Ukumbi: Mandalay Bay, Las Vegas (Machi, 2008)

Taji: WBC Super-featherweight

Katika pambano lililopewa jina la ‘Unfinished Decision’ ilikuwa mara yao ya pili kukutana na kwa hakika bado walikuwa na kazi ya ziada ya kumalizia. Manny aliomba pambano hili ili kumaliza ubishi wa lile la kwanza, ambalo wadau wengi walihisi ushindi wake haukuwa halali na kwamba Marquez alistahili. Kwenye raundi ya pili nusura Manny alambishwe sakafu kwa makonde mazito aliyotupiwa kwa mkupuo ila alistahimili vishindo na kulipiza kisasi kwa kumgonga Marquez KO kwenye raundi ya tatu. Raundi ya 10 Manny alimlewesha tena Marquez, ambaye alijizatiti katika raundi za mwisho kumdhuru mpinzani na kuwaacha uamuzi mgumu wa kufanya. Uamuzi huo wa majaji watatu ndio uliompa ushindi Manny akizoa alama 115-112, 114-113 na 112-115

Manny v Marcos Antonio Barrera

Ukumbi: Alamodrome, Texas (Jan. 2006)

Taji: Ring Magazine featherweight

Katika pambano hilo lililopewa jina la ‘Will To Win’, Barrera ndiye aliyekuwa akipewa nafasi ya kushinda kwa kuwa alikuwa amefanikiwa kwenye mapigano kadhaa ya nguvu. Kweli kwenye raundi ya kwanza, alimlambisha sakafu Manny. Pacman alijizoazoa na kwa kutumia kasi ya ngumi zake akalipiza kisasi raundi ya tatu kwa kumwangusha. Manny aliendelea na kasi yake na kufukia kwenye raundi ya 11, timu yake ikamwomba refa amalize pambano kwa kuwa Barrera alikuwa kaelemewa.

Manny v Erik Morales II

Ukumbi: Thomas and Mack Center, Las Vegas (Jan. 2006)

Taji: WBC Super Featherweight

Katika pambano hilo lililokwenda kwa jina la ‘The First One Was An epic’, alichokuwa akisaka Manny ni kulipiza kisasi baada ya Morales kumshinda kwa tofauti ya alama mwaka uliotangulia. Kama tu pambano la kwanza, Morales alikuwa moto kwa Manny na nusura amdondoshe mara mbili. Mara ya kwanza Manny alizuiliwa na kamba za uliongoni na mara ya pili kidogo amwangukie refa Bayless. Hapa Manny akaamua kutumia ujanja wake wa kurusha ngumi za kasi na ndicho kitu kilichomwokoa akimlambisha sakafu Morales kwenye raundi ya 10 na kuifuta kesi.