Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pablo: Simba hii unapigwa nyingi

SIMBA imepania. Inalitaka hili Kombe la Mapinduzi kutoka kwa mabingwa watetezi Yanga na katika kuthibitisha hilo, imeleta watu kwa ajili ya kuiongezea nguvu timu akiwamo winga wa kushoto kutoka Ivory Coast, Cheick Moukoro, 30, ambaye tayari yuko na kikosi mjini Zanzibar pamoja na kiungo wa zamani Sharaf Eldin Shiboub, aliyerejea kujaribiwa.

Moukoro na Shiboub walifuatana na kikosi kilichoondoka kwa boti, huku pia ikijiandaa kumleta Mkenya Harrison Mwendwa ambaye Mwanaspoti inafahamu kwamba Ofisa Mtendaji wa Klabu yake ya Kabwe Warriors ya Zambia yuko nchini akikamilisha mazungumzo ya uwezekano wa kuipata saini ya winga huyo.

Mwanaspoti inafahamu pia kuwa Simba ilituma maombi ya kumchukua kwa majaribio kiungo Mnigeria Udoh Etop kutoka katika klabu yake ya Arar ya Saudi Arabia, ambaye jana mchana alikuwa akifanyiwa vipimo vya Uviko-19 kwao Nigeria, huku pia kukiwa na mchezaji mwingine kutokea Senegal ambaye anatarajiwa kutua kuja kukiwasha kwenye Kombe la Mapinduzi.

Kocha wa wa Simba, Pablo Franco ameliambia Mwanaspoti kikosi chake kinaimarika na kwa nafasi ambazo wamekuwa wakitengeneza sasa, wakianza kuzitumia watakuwa ni moto wa kuotea mbali.

“Kwa kiasi kikubwa nimefanikiwa kuwapa falsafa zangu wachezaji kuwaelekeza tukiwa darasani pamoja na kiwanjani na mpaka sasa wamepokea kwa asilimia kama 60, sijui itakuwaje tukifika zaidi ya hapo,” alisema Franco na kuongeza;

“Nimevutia na uwezo walionao wachezaji wangu katika kupokea yale ninayowapatia, nimewaleza viongozi nahitaji wacheza 24, kwani hao ni rahisi kuwatawala, kuwaelekeza na wakaelewa kwa uarahisi kuliko kuwa na wimbo kubwa la wachezaji,”

“Maboresho ya wachezaji wachache tutakaowaongeza kwenye dirisha hili watakuwa ni wale wenye umuhimu kulingana na shida tulizokuwa nazo ndani ya timu na watakwenda kuongeza nguvu katika mahitaji yetu.

“Ukiangalia wakati huu ambavyo tunacheza tuna mbinu tofauti kwenye kushambulia hatutumii tena njia moja lakini kama haitoshi tumebadilika katika kuzuia.”


LWANGA KAREJEA

Pablo jana alifuatana na wachezaji 24 kwenda Zanzibar kwa ajili ya Kombe la Mapinduzi, ambako watatupa karata yao ya kwanza kesho Jumatano dhidi ya Selem View.

Kwenye msafara huo wa Simba kuna urejeo wa kiungo mkabaji, Taddeo Lwanga ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda usipungua miezi miwili kutokana na majeraha ya mguu yaliyokuwa yakimsumbua hadi akarudi kwao Uganda kwa matibabu zaidi.

Lwanga aliliambia Mwanaspoti ambalo liliweka kambi hapo Bandarini wakati wanaondoka kuwa maendeleo yake ni mazuri tofauti na wakati wa mwanzo.

Lwanga alisema amerejea akiwa vizuri na amepata ruhusa kutoka kwa madaktari waliokuwa wakimtibia na sasa anaweza kufanya mazoezi ya aina mbalimbali pamoja na wenzake na hata kuanza kucheza mechi.

“Maendeleo yangu ni mazuri mno hata kwa upande wangu nimejisikia faraja lakini kurejea na kucheza kwa nguvu kama awali si rahisi kufikia kule ila nitaanzia chini sababu sijacheza mechi muda mrefu na hata kuwa na timu pamoja,” alisema Lwanga.

Katika hatua nyingine kocha wa Simba, Pablo Franco alisema anategemea kumtumia Lwanga taratibu katika mazoezi na mechi za mashindano hayo ili kuona utimamu wake wa mwili na kumrudisha katika hali ya ushindani.

“Lwanga alikuwa nje kwa muda mrefu, si rahisi kucheza katika kiwango cha juu kama zamani, bali nitamtumia kidogo kidogo ili kumrudisha katika hali ya kujiamini na kupata muda zaidi wa kucheza,” alisema Pablo na kuongeza;

“Wachezaji wengine Erasto Nyoni na Israel Patrick Mwenda hawa nao walikuwa nje ya uwanja kwa sababu ya majeraha nao wamejiunga na timu nitakwenda kuwatumia katika mashindano haya taratibu ili kurudi katika ubora wao.”