Pablo: Hakuna pengo Simba
Maisha ya Bernard Morrison yamefikia mwisho ndani ya kikosi cha Simba. Kocha wa Simba, Pablo Franco amewatoa hofu mashabiki kwamba hakutakuwa na pengo lolote kikosini.
“Katika mechi na Pamba kuna Yusuph Mhilu ambaye ni mchezaji kijana na amefanya vizuri kwa kufunga mabao mawili pamoja na kutengeneza nafasi za kufunga naamini ana uwezo wa kufanya zaidi,” alisema Pablo na kuongeza;
“Wachezaji kama Kibu Denis, Pater Banda na wengineo wanaocheza kwenye nafasi hiyo naamini watafanya kazi kubwa zaidi ya wakati huu kwa kutimiza majukumu ya nafasi hiyo ili kumaliza vizuri msimu,” alisema.
Katika hatua nyingine Pablo alisema anaweza kubadili mfumo akatumia kiungo mwenye asili ya kati kwenda kucheza pembeni na mambo yakaendelea kuwa mazuri.
“Nadhani ni wakati sahihi wa kuheshimu uamuzi wa uongozi kwani Simba imesajili wachezaji wengi wenye uwezo wa wapo tayari kushindana muda wote na wana uwezo wa kuhakikisha tunashinda,” alisema Pablo na kuongeza;
“Jambo lingine zuri kwa timu kulikuwa na wachezaji wengi majeruhi ila wamerejea kama Sadio Kanoute na Taddeo Lwanga wataongeza nguvu katika kikosi.”