Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

OSCAR: Nani? Debora! Kuna Mwambungu 

Oscar Pict
Oscar Pict

Muktasari:

  • Watoza ushuru wa Kinondoni, KMC, walivutiwa na kipaji chake na kuamua kumrejesha nchini kwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuziba pengo la kinara wao wa upachikaji mabao msimu uliopita, Wazir Junior.

OSCAR Paul siyo jina geni katik Ligi Kuu Bara, aliyeanza kukipiga Tanzania Prisons kabla ya kutupiwa virago baada ya mkataba wake kwisha na kujiunga na Kakamega Home Boys ya Kenya.

Watoza ushuru wa Kinondoni, KMC, walivutiwa na kipaji chake na kuamua kumrejesha nchini kwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuziba pengo la kinara wao wa upachikaji mabao msimu uliopita, Wazir Junior.

Oscar bado hajaonyesha makali, lakini amefunguka kuwa ni suala la muda na timu yote kwa ujumla kufanya mambo makubwa ambayo yataifanya ifikie malengo kwa kumaliza nafasi tano za juu kwenye msimamo.

Mwanaspoti limefanya mahojiano na mshambuliaji huyo ambaye amefunguka mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumtaja Kenny Ally Mwambungu, kiungo wa KMC kwamba ni bora kuliko Debora Mavambo wa Simba, huku  straika Clement Mzize akitaka aaminiwe zaidi ndani ya kikosi cha Yanga.

OS01
OS01

DEBORA? KUNA MWAMBUNGU

Kwenye kikosi cha Simba jina linalotajwa mara kwa mara na mashabiki zao kutokana na ubora wake ni Debora Fernandes ambaye amesajiliwa msimu huu basi kwa upande wa mshambuliaji wa KMC, Oscar anasema anaheshimu kipaji chake, lakini anamkubali zaidi Kenny Ally Mwambungu.

“KMC kuna kina Fernandes wengi sana, lakini watu hawawaoni wanathamini wachezaji wa kigeni. Kwa upande wangu naamini Mwambungu ana uwezo mkubwa sana na anajua mpira," anasema na kuongeza:

"Ningekuwa kocha na nina wachezaji hao wawili anaanza Kenny. Sio kwa sababu Mwambungu ni mzawa, hapana. Nathamini kipaji chake, ana uwezo mkubwa sana ni mchezaji ambaye ni mpambanaji na ana pumzi.”

OS02
OS02

MZIZE ANATOSHA YANGA

Clement Mzize licha ya kutokuwa na namba nzuri za ufungaji tangu apandishwe Yanga akitokea timu ya vijana, lakini anatajwa kuwa mchezaji mwenye uwezo mkubwa ndani ya timu hiyo kama anavyodai Oscar.

“Yanga inawashambuliaji wengi wazuri kama Jean Baleke, Prince Dube na Mzize lakini mimi nikipewa nafasi ya kupanga kikosi hasa eneo la ushambuliaji naanza na Mzize kwa sababu ni mshambuliaji ambaye anaweza kuniofa vitu vingi uwanjani tofauti na hao wengine,” anasema.

“Sioni kwamba Baleke, Dube na Keneddy Musonda hawawezi mpira, ila naamini Mzize ana vitu vingi vizuri kuwazidi kwani ni mshambuliaji ambaye haogopi, anatumia nguvu na amekuwa mshindani hakubali kushindwa, anakaba na kushambulia.”

OS03
OS03

AUCHO NGUVU, AKILI

Kiungo mkabaji wa Yanga, Khalid Aucho amekuwa akitajwa kwa ubora na mashabiki wengi wa soka nchini kutokana na kutengeneza utulivu eneo analocheza ikiwa ni pamoja na kujenga ukuta mgumu akisaidiana na mabeki kina Ibrahim Hamad ‘Bacca’, Dickson Job kama anasema Oscar kuwa mchezaji anatakiwa kutumia akili na nguvu.

“Anatumia nguvu na akili, mchezaji ukiingia kinyonge unaumia. Ili kumuwini unatakiwa kuingia akifika na wewe unatakiwa kufika, lakini nguvu na akili muhimu kutokana na staa huyo kuwa fiti,” anasema Oscar.

“Kumkaba unatakiwa kujipanga ni aina ya wachezaji wachache wanaocheza ligi yetu. Navutiwa na aina yake ya uchezaji rafu zake sio za makusudi, wachezaji wakiingia vibaya kwa kumkaba bila ya kutumia nguvu na akili wanaumia wao.”

OS04
OS04

KMC WATAWASHANGAZA

KMC hawana msimu mzuri kutokana na kuanza vibaya ligi, lakini hilo upande wa Oscar ni suala la muda na watafanya mambo makubwa kutokana na aina ya kikosi walicho nacho.

“Ligi msimu huu ni ngumu, kila timu ni imara ukifanya kosa unaadhibiwa. Mwanzo (KMC) sio mzuri lakini nina imani kubwa na wachezaji wenzangu waliopo kwenye michezo iliyobaki tukiuma meno tutafikia malengo,” anasema.

“Nafikiri damu ilikuwa bado haijachanganya, (lakini) kadri tunavyocheza tunaongeza vitu vizuri na kupunguza makosa. Naamini tutakuwa bora na timu shindani ni suala la muda tu.”

OS05
OS05

YANGA ILIKUWA FAINALI

Mabao 5-0 waliyopigwa KMC msimu uliopita kumbe bado yanawatesa wachezaji na ndio sababu ya kucheza kwa ubora msimu huu wakipunguza idadi ya mabao kwa kuchapwa bao 1-0 kama anavyodai Oscar akisisitiza kuwa mchezo wao na Yanga ilikuwa fainali.

“Sikuwa sehemu ya kikosi kilichofungwa mabao 5-0 (msimu uliopita), lakini nimepata taarifa kutoka kwa wachezaji (wenzangu) kutokana na namna ambavyo tulikuwa tunahimizana kuhakikisha tunacheza vizuri na kutokubali kuendelea kuwa wanyonge,” anasema mchezaji huyo.

“Mechi tuliyopoteza kwa bao 1-0 (dhidi ya Yanga) tuliumia sana kwani tulijiandaa vyema. Tulicheza kama ndio mchezo wetu wa mwisho msimu huu. Kosa moja lilituadhibu.

“Mipango ilikuwa ni kukusanya pointi tatu mbele ya mabingwa watetezi. kwa namna moja tulifanikiwa lakini kosa moja tulilolifanya liliharibu mipango yote.”

OS06
OS06

ATAMANI REKODI ZA BOCCO

Kwa washambuliaji wanaocheza Ligi Kuu Bara upande wa wazawa, John Bocco ndiye mwenye rekodi nzuri katika upachikaji wa mabao na amekuwa kivutio kwa wachezaji wengine wanaocheza eneo hilo na Oscar  anasema: “Navutiwa na Cristian Ronaldo kwa mastaa wanaocheza soka nje ya Tanzania kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuona goli, lakini kwa wazawa natamani kufikia rekodi za Bocco.

“Bocco ndiye mshambuliaji ambaye nimekuwa nikimtazama. Najifunza mambo mengi kutoka kwake na kupitia mafanikio aliyo nayo natamani kupita njia zake ili niweze kucheza kwa kiwango chake na kufikia rekodi zake.”