Prime
Okello amgusa Aziz KI
WAKATI huu msimu wa 2025-2026 ukiwa umemalizika, ukiwauliza mashabiki wa Yanga kuna kitu gani watakimisi basi lazima watakutajia mabao ya kiungo wao Allan Okello na shangilia yake. Lakini sasa staa wao wa zamani Stephanie Aziz KI ameshangaa sana kiwango cha raia huyo wa Uganda.
Aziz KI yupo nchini na amekuwa akifutilia mechi za mwisho za Yanga wakati inafunga msimu na alipomuona Okello hakusita kuonyesha mshangao wake akisema jamaa ni fundi anayejua boli
Aziz KI aliliambia Mwanaspoti kuwa, Yanga kama ilitumia gharama kubwa za kumnasa kiungo huyo basi zilikwenda kihalali kwani ubora wake ni wa juu sana akijua kufunga na kutengeneza.
“Ukiniuliza ni kitu gani kimenifurahisha nitakwambia kuona Yanga inatetea ubingwa wake lakini kitu kilichonivutia zaidi ni kiwango cha huyu Okello ni mchezaji bora sana,” amesemaAzizi KI.
“Kwanza nimependa anatumia mguu wa kushoto kama Mimi lakini anajua sana anafunga na kutengeneza nafasi ni mchezaji wa kiwango cha juu sana amenivutia sana.
“Nadhani hapa klabu yangu na viongozi wangu wa zamani walifanya kazi nyingine nzuri ya kumpata mchezaji mkubwa mwenye kipaji ambacho hakina maswali.”
Okello ndiye amemaliza kinara wa ufungaji kwenye kikosi Cha Yanga akimaliza na mabao 14 akiyafunga kwenye nusu msimu tu tangu asajiliwe dirisha dogo la Januari msimu uliopita.
Mbali na kujua kufunga Okello pia amefanikiwa kutengeneza asisti nane na kumfanya kuhusika kwenye jumla ya mabao 22 kwenye kikosi cha mabingwa hao wa Ligi Kuu ya NBC.
Aidha Azizi KI hakusita kuweka wazi kwamba licha ya Yanga kumaliza msimu na ubingwa wa tano mfululizo lakini wachezaji wa kikosi hicho wanahitaji mapumziko kutokana na kuonekana kuwa na uchovu mkubwa.
“Yanga wametetea ubingwa lakini ukweli ni kwamba wachezaji wamechoka sana, Wana uchovu mkubwa, wanastahili mapumziko ili waweze kurudisha utulivu wa miili yao, wengi ni wale ambao wamecheza sana misimu mitatu hii.
“Wanahitaji kupongezwa sana kwa namna walivyojutuma na kutetea ubingwa huu msimu umekwisha wapumzike kabisa ili waweze kurudi na nguvu msimu ujao.”