Nyota wanne Yanga watua Z’bar Heroes

Muktasari:
- Timu hiyo ya visiwani inasaka taji la pili la mashindano ya Chalenji msimu huu
Wachezaji wanne wa Yanga wamejiunga na kikosi cha Zanzibar Heroes kujiandaa na mashidano ya Chalenji yanayotarajiwa kufanyika Desembe 3, nchini Kenya.
Wachezaji wa Yanga waliojiunga na kikosi hicho ni washambuliaji Emmanuel Martin, Mateo Anton na mabeki Haji Mwinyi Ngwali, Abdallah Haji Shaibu ‘Ninja’.
Kocha Mkuu wa timu ya ‘Zanzibar Heroes’ Hemed Morocco alisema anaimani ujio wa wachezaji hao umeongeza nguvu katika kikosi chake kuelekea katika mashindano ya Chalenj.
“Tunaimani wachezaji tuliowateuliwa kutoka klabu za Tanzania Bara watakuwa na msaada mkubwa kwetu katika mashindano haya,”alisema Morocco.
Wachezaji wanaocheza Bara waliokuwa katika kikosi cha Z’bar Heroes ni pamoja na Nassor Mrisho ‘Okapi’, Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Abdulla Kheir "Sebo" (Azam), Mohd Issa "Banka" (Mtibwa Sugar), Mbarouk Marshed (Super Falcon), Suleiman Kassim "Selembe" (Majimaji) pamoja na Kassim Suleiman (Prisons).