Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota Serengeti Boys huyoo Denmark

Muktasari:

Wachezaji wa Serengeti Boys wameonyesha kiwango cha kuvutia katika mashindano mbalimbali ambayo wameshiriki wiki hivi karibuni kiasi cha wadau na mashabiki wa soka kutamani timu hiyo kuwa hata timu ya Taifa.

NEEMA imezidi kukiangukia kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana U-17, Serengeti Boys baada ya nahodha wake, Maurice Abraham kupata zali la kwenda Denmark.

Maurice a.k.a Chuji alionyesha kiwango kizuri katika michuano ya kuwania Afcon 2019 Kanda ya Cecafa, ambapo Serengeti ilimaliza nafasi ya tatu.

Kocha Mkuu wa Serengeti, Oscar Mirambo, aliliambia Mwanaspoti kuwa, Chuji ataondoka nchini hivi karibuni baada ya kupata mualiko wa kwenda kufanya majaribio Denmark.

“Sio kweli eti anaenda Manchester Utd kama watu wanavyosema, ila mialiko ipo mingi kwa vijana lakini Maurice, viza yake ishapatikana na ataondoka kwenda Denmark Oktoba 7,” alisema.

Mirambo alisema nyota wengi wa kikosi hicho cha vijana, kitakachokuwa wenyeji wa Fainali za Afcon 2019 wataondoka kwa utaratibu kama uliofanywa kwa Maurice.

“Mialiko ipo mingi na baadhi ya wachezaji ila siwezi kusema nani anafuata sasa, lakini Maurice ameanza na tunasubiri taratibu zikamilike kwa wengine ndipo tutaweka wazi,” alisema kocha huyo ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania.