Nyambaya, Oscar Oscar wajitosa TFF

Muktasari:
- Uchaguzi huo utafanyika Agosti 7, ukitanguliwa na matukio mbalimbali ikiwamo usaili utakaofanyika kwa siku tatu kuanzia Juni 25 na Agosti Mosi hadi 6 wagombea watafanya kampeni tayari kwa uchaguzi.
Mambo yanazidi kunoga kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya Lameck Nyambaya na Oscar Oscar kujitosa kwenye kinyang'anyoro hicho.
Nyambaya ambaye ni mwenyekiti wa wa Chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na Osacar wamechukua fomu leo Juni 9.
Nyambaya anawania ujumbe wa kamati tendaji, wakati Oscar amejitosa kuwania urais.
Kujitokeza kwa wagombea hao ni muendelezo wa wadau wa soka kujitosa kwenye kinyang'anyiro hicho tangu kufunguliwa kwa pazia la kuchukua na kurejesha fomu jana.
Awali, rais anayetetea kiti chake, Wallace Karia, Evans G Mgeusa na Zahor Mohammed Haji walifungua dimba la kuchukua fomu wote wakiwania urais wa TFF.
Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu litafungwa saa 10 jioni ya Juni 12 tayari kwa uchaguzi huo utakaofanyika mkoani Tanga Agosti 7.