Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nooij: 4-3-3 iliichakaza Zimbabwe

KOCHA wa Taifa Stars, Martinus Nooij.PICHA|MAKTABA

Muktasari:

  • Nooij aliitaja mfumo aliotumia katika mchezo huo na kudai kuwa ndiyo uliofanikisha kuibuka kidedea kuwa ni 4-3-3.

KOCHA wa Taifa Stars, Martinus Nooij amefichua siri ya kikosi chake kulazimisha sare ya mabao 2-2 ugenini dhidi ya Zimbabwe katika pambano la kusaka tiketi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika lililopigwa Juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Harare.

Nooij aliitaja mfumo aliotumia katika mchezo huo na kudai kuwa ndiyo uliofanikisha kuibuka kidedea kuwa ni 4-3-3.

“Nilifahamu wazi wapinzani wetu watataka kutushambulia sana kwavile wako nyumbani  ili wapate mabao ,hivyo nilihakikisha naimarisha kiungo ambacho katika mchezo wa Dar es Salaam hakukicheza sawasawa.

“Nilianza na viungo watatu, Erasto(Nyoni), Kazimoto (Mwinyi) na Amri Kiemba ambaye alikuwa  anacheza nyuma ya John Bocco lakini wakati mwingine alikuwa anashuka chini kwaajili ya kusaidia kukaba kwa kiasi kikubwa hapa tulifanikiwa na timu ilitengeneza nafasi za kufunga,”alisema Nooij

Aliongeza: “Tulianza na mfumo wa 4-3-3, yaani mabeki wanne, viungo watatu na washambuliaji watatu,lakini kipindi cha pili nilibadili mfumo wakati ambao matokeo yalikuwa 2-2, nilimtoa Msuva na kumwingiza Said Morad. Niliimarisha ulinzi hivyo mabeki wakawa watano, Canavaro, Kelvin Yondani, Oscar Joshua, Shomari Kapombe na Morad na matokeo kuwa mazuri kwa upande wetu,”.

Akizungumzia sababu ya kumuanzisha Msuva kama winga wa kulia badala ya Ngasa aliyemtumia kwenye mchezo wa kwanza Nooij alisema: “Nilitaka watu ambao wanaweza kusaidia kukaba pia ndiyo maana nilianza na Msuva na kwa kweli alijitahidi kuifanya kazi yake sawasawa.”