Njombe ikiwadaka hawa, siyo mchezo

Muktasari:
Meneja wa mchezaji huyo aliyejitambulisha kwa jina la Oscar alisema leo asubuhi wameondoka wachezaji wake wawili kwenda Njombe, kwaajili ya kwenda kumalizana na viongozi wa timu hiyo.
Dar es Salaam. Kiungo wa zamani wa African Lyon, Awadh Salum yupo mbioni kutua Njombe Mji baada ya uongozi wa timu hiyo kuonyesha nia naye kwa kumtumia pesa ya nauli kwenda kufanya mazungumzo.
Meneja wa mchezaji huyo aliyejitambulisha kwa jina la Oscar alisema leo asubuhi wameondoka wachezaji wake wawili kwenda Njombe, kwaajili ya kwenda kumalizana na viongozi wa timu hiyo.
“Ni kweli ameondoka Awadh pamoja na Raphael Siame hawa wote ni wachezaji wazuri, wataisaidia Njombe kwasababu bado ni vijana wadogo, Njombe walituma tiketi zao kikubwa walitaka kuwaona na kisha kusaini, ila sina wasiwasi kwasababu wao wote wanawafahamu wachezaji hawa,”alisema meneja huyo.
Wachezaji hao walisema kuwa wanaenda Njombe kupambana na siyo kuuza sura na hawatoitumia nafasi hiyo vibaya kwani wameaminiwa sana na viongozi wa timu hiyo kwani hata Njombe kuna wachezaji lakini wameaminiwa wao.