Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makocha Ligi ya U20 hamna baya wanangu

Muktasari:

  • Timu nne zilizoingia nusu fainali ambazo ni Azam FC, Kagera Sugar, KenGold na Fountain Gate kwa hakika zimetupa ladha sana hapa kijiweni kutokana na timu zilivyoonyesha viwango vizuri na ushindani wa hali ya juu.

SOKA limepigwa hasa katika 8-Bora ya Ligi Kuu ya soka kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20 nchini na mvuto zaidi ulikuwa kwenye nusu fainali.

Timu nne zilizoingia nusu fainali ambazo ni Azam FC, Kagera Sugar, KenGold na Fountain Gate kwa hakika zimetupa ladha sana hapa kijiweni kutokana na timu zilivyoonyesha viwango vizuri na ushindani wa hali ya juu.

Wachezaji wameonyesha uwezo mkubwa wa kutafsiri mambo manne ya msingi ambayo katika soka la kisasa ndio yamekuwa yakitoa muelekeo na kuamua matokeo ya mchezo wa mpira wa miguu.

Mambo hayo manne ni timu inapokuwa na umiliki wa mpira, inapokuwa haimiliki, inaposhambuliwa na inaposhambulia ambapo kila mchezaji anapaswa kufahamu wapi anapaswa awepo na nini akifanye ili kuhakikisha timu ipo salama.

Katika soka la kisasa, hayo ni mambo ya msingi ambayo wachezaji wanapaswa kufundishwa na kuyafahamu wakiwa katika umri mdogo ili kuwafanya wawe bora zaidi pale wanapofikisha umri wa kutegemewa katika vikosi vya wakubwa hivyo inatia faraja kuona vijana wakimudu hilo katika ligi yao hapa nchini.

Bahati nzuri makocha ambao wanazifundisha timu hizo, wengi ni vijana jambo linalotoa ishara njema kwamba muelekeo wa soka letu ni mzuri na nchi itakuwa na makocha wengi wazuri siku za usoni ambao wataweza kushindana sokoni na makocha wa kigeni.

Vijana wa Azam wenyewe wamenolewa na kocha Kassim Liogope, Kagera Sugar wapo chini ya Salim Mbonde, KenGold wanaongozwa na Anthony Mwamlima ‘Noriega’ wakati huo Fountain Gate wako chini ya Abubakary Ally.

Kijiwe kinawatakia kila la kheri katika fani ya ukocha na kinaamini kile ambacho wamekionyesha katika Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 kitakuwa na muendelezo na watakuwa na msaada mkubwa kwa nchi siku za usoni.

Wahenga walisema hata mbuyu ulianza kama mchicha hivyo tuna matumaini makubwa makocha hawa watafikia nchi ya ahadi.