Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ninje apewa shavu jingine TFF

KOCHA Ammy Ninje ameula baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), huku nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya shirikisho hilo iliyoachwa wazi na Revocatus Kuuli ikipata mrithi.

Ninje amechukua nafasi hiyo iliyokuwa ikikaimiwa na Oscar Milambo anayeinoa timu ya Vijana U17, Serengeti Boys.

Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokutana Jumamosi ya Oktoba 20 kilipitisha maamuzi hayo.

Ndimbo alisema Kamati ya Utendaji imefanya mabadiliko ya baadhi ya kamati na Kamati ya Nidhamu itaongozwa na Kiomoni Kibamba, Peter Hella, Kassim Dau, Handley Matwenga na Twaha Mtengera.

Kamati ya Maadili, Richard Mbaruku, Thadeus Karua, Mussa Zungu, Benedict Nyagabona na Lugano Hosea.