Ni vita ya Mukoko na Tadeo

MECHI ya watani wa jadi, Simba dhidi ya Yanga inachezwa kesho saa 11:00 jioni katika uwanja wa Benjamin Mkapa, lakini katika mchezo huo kutakuwa na vita kubwa katika eneo la kiungo.

Vita ya kiungo ambayo inatarajia kutokea katika mchezo huu ni upande wa eneo la ukabaji baada ya timu zote mbili kuwa na viungo wenye uwezo wa juu.

Simba kwenye eneo la ukabaji wana Tadeo Lwanga ambaye ana uwezo mkubwa wa kukaba, staili yake ikiwa ni kutumia nguvu zaidi.

Yanga wao katika eneo hilo yupo Tonombe Mukoko ambaye ana ubora wa hali ya juu katika kukaba na kuituliza timu pindi inaposhambuliwa.

Viungo wote hawa wana mchango mkubwa katika timu zao kuhakikisha viungo washambuliaji wanafanya kazi yao kwa ufasaha wa hali ya juu.

Katika mchezo wa kesho eneo ambalo litakuwa na mvutano zaidi ni kwenye kiungo kwani ndio sehemu ambayo inahusika katika kuanzisha mashambulizi.