Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni Tshishimbi na Klaus Kindoki tu

Muktasari:

Katika hatua njyingine Mwakalebela alisema nyota wao wanatarajia kuingia kambini Julai 7, mwaka huu tayari ili kujiweka fiti kwa mchezo wa kirafiki wa kutambulisha nyota wao wapya zoezi litakalofanyika Julai 27.


HAKUNA ubishi tena, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe hawataonekana tena wakiwa na uzi wa Jangwani baada ya mabosi wa klabu hiyo kutangaza mapro wakigeni wawili tu, akiwamo kipa Klaus Kindoki na kiungo Papy Kabamba Tshishimbi, huku wakiachana rasmi na Ibrahim Ajibu.

Hata hivyo, Kindoki yupo mbioni kutolewa kwa mkopo katika Klabu ya Singida United kwa njia ya kuacha nafasi kwa Farouk Shikalo kutoka Kenya ambaye Kocha Mwinyi Zahera amemalizana naye walipokutana Hispania.

Katika msimu uliopita, Yanga ilikuwa na nyota watano wa kigeni akiwamo Heritier Makambo aliyesajiliwa na Horoya AC ya Guinea, Kamusoko, Tambwe, Kindoki na Tshishimbi aliyeongezewa mkataba wa miaka miwili ndani ya klabu hiyo.

Mwanaspoti limepenyezewa habari za ndani kutoka Yanga kwamba Kindoki atalazimika kwenda Singida United ili kumpisha Shikalo, huku mabosi wa klabu hiyo wakitangaza rasmi kuachana na Ajibu aliyesajiliwa Simba kwa mkataba wa miaka miwili.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema wamekaa muda mrefu na Ajibu kwa lengo la kumuongeza mkataba lakini wameshindwana.

“Ajibu ni mchezaji mzuri na kila timu inatamani kuwa naye katika kikosi chake lakini ndiye mwenye uamuzi wa kucheza timu anayoitaka milango ipo wazi kwake kama atahitaji kuendelea nasi au kuondoka,” alisema.

Katika hatua nyingine alisema baada ya kuanza na usajili wa nyota wa ndani kwa kuanza na Ally Ally sasa wapo katika michakato ya kuzungumza na nyota wao waliomaliza mikataba na huenda ndani ya wiki ijayo watakuwa wamemalizana na baadhi yao.

“Tumeamua kuweka wazi ishu za Ajibu kwa vile ndiye mchezaji aliyekuwa anauliziwa mara kwa mara na kuhusiana na nyota wengine ambao wamemaliza mikataba na sisi tuna mipango nao tumeshaanza mazungumzo tukikamilisha kila kitu kitakuwa wazi,”

Katika hatua njyingine Mwakalebela alisema nyota wao wanatarajia kuingia kambini Julai 7, mwaka huu tayari ili kujiweka fiti kwa mchezo wa kirafiki wa kutambulisha nyota wao wapya zoezi litakalofanyika Julai 27.

“Tutakuwa na Tamasha la Siku ya Mwananchi ambalo ni maalumu kwa shughuli za kijamii na kutambulisha kikosi chetu cha msimu ujao tutachangia damu, kutembelea vituo vya watoto yatima na kufanya usafi maeneo ya Jiji la Dar es Salaam.”