Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kagera Sugar ina mtego wa miaka 21

KAGERA Pict

Muktasari:

  • Ligi hiyo ilisimama kwa muda kupisha kalenda ya kimataifa, kisha kurejea kwa Simba kucheza viporo vyake dhidi ya Mashujaa, JKT Tanzania, Pamba Jiji iliyocheza nao jana na keshokutwa itamalizana na KMC kabla ya klabu nyingine kuingia raundi ya 28 ikiwa ni lala salama ya msimu huu wa 2024-2025.

WAKATI Ligi Kuu Bara ikirejea tena wikiendi hii baada ya kushuhudiwa viporo vinne vya mechi za Simba vikimalizika, Kagera Sugar ipo katika mtego wa kukwepa aibu ya miaka 21 katika ligi hiyo.

Ligi hiyo ilisimama kwa muda kupisha kalenda ya kimataifa, kisha kurejea kwa Simba kucheza viporo vyake dhidi ya Mashujaa, JKT Tanzania, Pamba Jiji iliyocheza nao jana na keshokutwa itamalizana na KMC kabla ya klabu nyingine kuingia raundi ya 28 ikiwa ni lala salama ya msimu huu wa 2024-2025.

Hadi sasa ni timu tisa za juu pekee zimeshajihakikishia kubaki Ligi Kuu msimu ujao, huku nyingine saba zikiwa na presha kubwa kukwepa kushuka daraja.

Tayari KenGold imeshaaga mashindano hayo kwa kushuka daraja na pointi 16 na sasa inamalizia mechi zake zilizobaki ili kujiandaa na Championship msimu ujao ili kuona namna ya kurudi tena 2026/27.

Kati ya timu saba ambazo presha ni kubwa, nne ndizo viroho vinadunda zaidi kukwepa mtego wa kuungana na KenGold, ikiwa ni Pamba Jiji yenye pointi 27 nafasi ya 13 sawa na Prisons nafasi ya 14.

Kagera iliopo nafasi ya 15 imekusanya alama 22 na macho na masikio ya wengi wanasubiri kuona iwapo wakongwe hao itashuka au kubaki baada ya kudumu Ligi Kuu miaka 21 tangu walipopanda 2004.

Timu hiyo pekee ya mkoani Kagera imekuwa na historia tofauti na iliwahi kumaliza nafasi nne za juu msimu wa 2016/17 huku ikiponea chupuchupu kushuka 2018/19 kwa kushinda play off dhidi ya Pamba kwa jumla ya mabao 2-0.

Kwa sasa timu hiyo inanolewa na nyota wake wa zamani aliyewahi kukipiga Simba, Yanga na timu ya Taifa, Taifa Stars, Juma Kaseja inahitaji pointi tisa kati ya mechi tatu zilizobaki kujua hatma yake.

Wengine ni Pamba iliyopanda msimu huu na kati ya mechi tatu zilizobaki inahitaji alama nne ili kuwa salama la sivyo huenda ikarudi ilipotoka kuanza kujipanga upya msimu ujao wa Championship.

Ligi hiyo inatarajia kuendelea Machi 13 na Tanzania Prisons itakuwa nyumbani dhidi ya Coastal Union na kama itapoteza huenda matumaini ya kubaki Ligi Kuu yakapotea na kufanya presha kuwa juu kukwepa aibu ya kushuka daraja.

Hata hivyo, wakati Maafande hao ikisaka alama tatu, ikifanikiwa, huenda ikaiweka Kagera sehemu mbaya kwenye kushuka daraja, huku ‘Wanankurukunbi’ hao ikiweka matumaini katika mechi yao dhidi ya Mashujaa, Namungo na Simba kuona ikishinda.

Pamba Jiji baada ya mchezo wa jana dhidi ya Simba, itakuwa na dakika 270 za jasho na damu dhidi ya KenGold Mei 13 Sokoine Mbeya, kisha kurudi Kirumba dhidi ya JKT Tanzania na KMC kujiuliza hatma yake.

Timu nyingine ambazo hazipo salama sana ni Fountain Gate iliyo nafasi ya 12 na alama 29, KMC na Mashujaa zilizovuna alama 30 kila mmoja na kufanya upinzani kuwa mzito kupambania nafasi ya kubaki Ligi Kuu.

Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Aman Josiah alisema bado haijaisha hadi iishe akiomba sapoti ya mashabiki kuhakikisha dhidi ya Coastal Union wanashinda kabla ya kuikabili Yanga na kumalizia msimu dhidi ya Singida Black Stars.

“Huu ndiyo muda wa kuonyesha tunachotaka, hatuhitaji sare kwa sasa zaidi ya pointi tatu, tunajua dakika 270 zilizobaki ni jasho na damu lazima tupambane kila mmoja ajitoe kwa nafasi yake kupigania nembo hii,” alisema Josiah.

Kocha Mkuu wa Kagera, Juma Kaseja alisema; “Bado ni mapema mechi zilizobaki tunahitaji ushindi bila kujali nani tunacheza naye au yuko wapi, ninayo matumaini na vijana wangu kuweza kupambana kama walivyofanya nyuma, tunaomba utulivu mazuri yapo” alisema Kaseja.