Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nataka kuweka historia Yanga!

Edward Chal

Muktasari:

Manyama ambaye anataka kuvaa jezi namba 28 kwenye kikosi cha Yanga, JKT Ruvu alikuwa akivaa namba 27.

YANGA imefanya kweli baada ya kumnasa kiraka, Edward Charles Manyama ambaye amewatamkia mabosi wake hao wapya kamwe hawatajutia usajili wake.

Manyama ambaye anataka kuvaa jezi namba 28 kwenye kikosi cha Yanga, JKT Ruvu alikuwa akivaa namba 27.

Inawezekana sababu ya kuchagua namba 28 ni baada ya 27 kumilikiwa na mshambuliaji, Simon Msuva na itakuwa ngumu kumwachia. Amesema moja ya malengo aliyojiwekea kwenye kikosi cha Yanga ni kuwa mchezaji wa kwanza mzawa kuuzwa nje ya nchi.

Manyama ambaye ana akili, kasi na nguvu ya mpira na umbile lake la kujazia na urefu uliompeleka hewani ‘Ngongoti’ unamfanya ubora wake uongezeke zaidi.

Wadau wa soka wanamtambua kwa uwezo wake wa kucheza beki wa kushoto lakini ni kiraka mzuri sana kwani akipewa nafasi ya kucheza kiungo mkabaji au beki ya kati utamsahau, ana uwezo wa juu sana.

Na hicho ndiyo kimewashawishi makocha na benchi la ufundi la Taifa Stars wawe naye kikosini hadi sasa. Hana muda mrefu kwenye soka kwani ameichezea JKT Ruvu kwa nusu msimu tu mzunguko wa pili akitokea kikosi cha vijana U-20 akaonyesha kiwango cha juu.

Klabu za Simba na Azam FC ndizo zilikuwa za kwanza kumnyatia, lakini dakika za mwisho akasaini Yanga kwa mkataba wa miaka miwili. “Mimi ni mchezaji, nimechagua maisha yangu ni mpira hivyo nina malengo yangu, naweza kusema tulishindwana kwenye masilahi,”anasema Manyama anayeishabikia klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani.

“Ninaamini nimefanya chaguo sahihi na nitatimiza malengo yangu kwenye kikosi hicho kwa kupambana na kupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.” Manyama ametua Yanga ambayo dhamira yao ni kumtumia kama beki wa kushoto ambako atapigania namba na Oscar Joshua.

“Pale naenda kupigania namba na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, naamini nitafanikiwa kwa sababu najua maisha ya mpira yanataka nini. Kuna mambo matatu ndiyo yataniongoza mimi kwanza ni kujituma, nidhamu na malengo wakati huo namwomba Mungu anijaalie afya na uzima,”anasema Manyama anayevutiwa na beki wa kushoto Muaustria David Alaba wa Bayern Munich.

“Akili yangu inaniambia nifanye kazi na kuwa mchezaji wa kwanza mzawa kuuza na Yanga nje ya nchi kwa sababu ya kipaji changu, naamini halitashindikana.”

Kuhusu kocha wake, Mbrazili Marcio Maximo amesema: “Ni kocha mzuri ingawa bado sijafanya kazi naye, lakini ninachoamini anataka kumtumia mchezaji mwenye uwezo, umakini na akili ya mpira kama nilivyodhamiria kufanya.”

Kihistoria awali alikuwa anawaficha wazazi wake juu ya kipaji chake na walikuja kugundua baada ya kumsikia redioni akitajwa na mtangazaji kwenye mechi za JKT walizocheza na Simba na Yanga.

Anasema, wazazi wake hao baba yake, Charles Manyama na mama yake Veronica Edward haishi nao wako mkoani Tabora. Dar alikuwa anasoma Shule ya Sekondari Makongo ambayo ndiyo ilimtambulisha alipokuwa aichezea mashindano mbalimbali hadi akasajiliwa na JKT Ruvu. Ni wa mwisho kuzaliwa kwenye familia yenye watoto wanne. Alisoma Shule ya Msingi Imeli ya Nzega, Tabora kabla ya kujiunga na Sekondari ya Makongo jijini Dar es Salaam na kuhitimu Kidato cha Nne mwaka jana.

Kipaji chake kilianza tangu utoto na alipokuwa shule ya msingi na timu yake ya mtaani ya Tiba FC alichaguliwa kwenye kikosi cha Copa Coca Cola Mkoa wa Tabora. Luteni Kanali Mwangasi ambaye pia ndiyo Mkuu wa Sekondari ya Makongo alimwona na kumwandikisha shuleni hapo.