Namungo watanguliza mguu makundi CAF

MECHI ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya CD de Agosto dhidi ya Namungo imemalizika kwa Namungo kuibuka na ushindi mnono wa bao 6-2.

Mchezo huo umepigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex bila Mashabiki wa aina yeyote huku Agosto wakiwa ndio wenyeji baada ya Shirikisho la Soka Afrika kuamua mechi zote mbili za timu hizi mbili kuchezewa nchini Tanzania baada ya Angola kytokea shida.

Agosto ndio walianza kupata bao dakika ya 11 kupitia kwa Brayan Moyo bao lilitokana na Penalti iliyopigwa na mchezaji mmoja wa Agosto na kupanguliwa na golikipa wa Namungo Jonathan Nahimana mpira ukamkuta mchezaji wa Agosto akapiga shuti lililookolewa tena na kipa huyo ukamkuta Moyo na kuuzamisha nyavuni.

Dakika ya 32 Namungo wamesawazisha kupitia kwa Hashimu manyanya aliyefunga kwa kichwa na kufanya ubao wa matokeo usomeke 1-1.

Wachezajo wa Namungo baada ya bao hilo waliendelea kulisakama lango la Agosto na dakika ya 38 kupitia kwa Sixitus Sabilo walipata bao la pili na la kuongoza.

Kipindi cha pili kilirejea kwa Namungo kufanya kwa kuwato Leriant Lusajo, Stive Nzigamasabo na Hashimu  Manyanya nafasi zao zikichukuliwa na Shiza Kichuya, Idd Kipwagile na Erick Kwizera walioonekana kuongeza presha langoni  kwa Agosto.

Dakika ya 51 CD de Agosto walipata bao la kusawazisha kupitia kwa Ambrosini Antonio kwa shuti kali bao ambalo halikudumu na dakika  ya 55 Leliant Lusajo aliwapatia Namungo bao la tatu.

Dakika ya 60 Namungo walipata  bao la nne kupitia kwa Sixitus Sabilo na dakika  ya 64 Erick Kwizera aliwapatia Namungo bao la tano na dakika ya 70 Stephen Sey aliweka nyavuni bao la sita kwa Namungo na la mwisho katika mchezo huo.

Dakika ya 83 kipa wa Namungo Jonathan Nahimana ameonesha umahiri wake kwa kudaka mkwaju wa penalti uliofungwa na moja ya wachezaji wa Agosto.

Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika ubao wa matokeo ulikuwa ukisomeka CD de Agosto 2-6 Namungo.

Mchezo wa marudiano utapigwe kwenye dimba hilohilo la Chamazi Alhamisi Februari 25.