Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namungo warejea Tanzania bila wenzao wanne

HATIMAYE msafara wa wachezaji wa Timu ya Namungo umeanza safari ya kutoka Hotelini kuelekea Uwanja wa Ndege nchini Angola kurudi Tanzania huku wanne wakiachwa karantini.
Namungo walikwama nchini humo kutokana na sintofahamu baada ya wachezaji wao watatu Lucas Kikoti, Fred Tangalu na Khamis Faki kudaiwa kuwa na virusi vya corona sambamba na Mtendaji Mkuu, Omary Kaaya.
Mkuu wa Idara ya habari ya klabu hiyo Kindamba Namlia ameiambia Mwanaspoti muda huu kuwa, kikosi hicho kipo njiani kurejea Tanzania huku wachezaji hao wakiachwa huko.
"Ndio timu inarejea Tanzania kuendelea na majukumu mengine, ila wale watu wetu wanne tumewaacha huko huko,"
"Wakikamilisha muda ambao wamejiwekea Nchini humo mara tu mtu akigundulika kuwa na Corona basi wanarejea Tanzania kwa gharama za Serikali ya Angola,"anasema.
Namlia anasema walichokifanya wapinzani wao Primeiro De Agosto ni jambo baya na la mipango kwa madai sio jambo la kawaida ambalo wamefanyiwa mpaka hivi sasa.