Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nabi atoa sababu kuikataa Azam FC

Muktasari:

  • Taoussi aliyetua juzi nchini sambamba na wasaidizi watatu, Kocha msaidizi, Ouajou Driss, Kocha wa utimamu wa mwili, Badr Eddine na Kocha wa Makipa, Rachid El Mekkaoui tayari wameanza kazi kuiandaa Azam kwa mechi za Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho baada ya kung’olewa michuano ya CAF.

AZAM FC imemtangaza Rachid Taoussi kuwa kocha mkuu kwa mkataba wa mwaka mmoja kuchukua nafasi ya Youssouf Dabo, lakini kabla ya kutua kwa Mmorocco huyo, ilidaiwa klabu hiyo ilikuwa ikimwinda kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi aliyefungua sababu ya kulitema dili ghilo la Chamazi.

Taoussi aliyetua juzi nchini sambamba na wasaidizi watatu, Kocha msaidizi, Ouajou Driss, Kocha wa utimamu wa mwili, Badr Eddine na Kocha wa Makipa, Rachid El Mekkaoui tayari wameanza kazi kuiandaa Azam kwa mechi za Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho baada ya kung’olewa michuano ya CAF.

Nabi aliyekuwa akitajwa angemrithi Dabo kabla ya jina la Florent Ibenge kuibuka baadae, lakini kuvuja kwa taarifa za kutakiwa kwake kulimfanya Mkongomani huyo kuchomoa akiamua kusalia Al Hilal, huku kocha wa zamani wa Yanga alifichua sababu iliyomzuia kujiunga na timu hiyo.

Mtunisia huyo aliyeweka rekodi tangu Ligi Kuu Bara akiwa na Yanga kabla ya kuondoka kwenda FAR Rabat na sasa kutua Kaizer Chiefs aliliambia Mwanaspoti ni kweli alishazungumza na mabosi wa Azam, lakini mkataba mpya na Amakhosi ulimfanya ajizuie kurejea nchini kufundisha.

Nabi alisema, Azam ni timu kubwa na anaifahamu vizuri kwa sababu amefundisha huko ligi ya Tanzania na kwamba ana mazungumzo mazuri na viongozi wa klabu hiyo, hivyo anafahamu kuwa ni miongoni mwa timu yenye malengo makubwa, lakini ilikuwa ngumu kuungana nao kwa sasa.

“Sababu kubwa ni moja tu, kwa sasa niko na Kaizer Chief ambayo ndiyo kwanza nimeanza kuifundisha hivyo siwezi kuachana nayo kirahisi wakati waliniamini kabla,” alisema Nabi aliyeiwezesha Yanga kucheza mechi 49 bila kupoteza na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho msimu miwili mfululizo.

“Kwa sasa nataka kuelekeza akili yangu kwenye kuibadilisha Kaizer, mashabiki wa timu hii wameonyesha kuwa na imani kubwa na kama nitaondoka kwangu naona ni kama kuwafanyia ukatili,” aliongeza Nabi.