Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nabi apangua saba akiikabili Biashara United, Mwamnyeto arejea

Yanga imefanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake kitakachoanza leo dhidi ya Biashara United ambapo jumla ya wachezaji saba walioanza katika mchezo uliopita wamepanguliwa.

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasredine Nabi amefanya mabadiliko makubwa ya kikosi kilichoanza katika mchezo uliopita dhidi ya Mbeya Kwanza ambao ni Djigui Diarra, Kibwana Shomari, Yanick Bangala, Khalid Aucho, Sureboy, Jesus Moloko na Saido Ntibazonkiza.

Baadhi ya nyota hao akiwemo Djigui Diarra, Sureboy na Yanick Bangala wamepumzishwa ambapo Mwanaspoti limeshuhudia wakiwa wamekaa jukwaani na baadhi ya viongozi wa klabu ya Yanga.

Nyota wengine ambao wamepanguliwa Khalid Aucho, Jesus Moloko, Saido Ntibazonkiza wakianzia kikosi cha akiba huku Kibwana Shomari aliyeanza katika mchezo uliopita akiwa siyo sehemu ya mchezo wa leo.

Katika mchezo wa leo Kocha Nabi ameanza na kipa Abdultwalib Mshery, Djuma Shaban, Yasin Mustapha, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Zawadi Mauya, Chiko Ushindi, Farid Mussa, Fiston Mayele, Feisal Salum na Dickson Ambundo.

Wachezaji wa akiba ni Erick Hola, Paul Godfrey, Khalid Aucho, Denis Nkane, Jesus Moloko, Heritier Makambo, Crispin Ngushi, Saido Ntibazonkiza na Ibrahim Abdallah.