Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

N’Golo Kante anaingia, anatoka Inter Milan

Inter Milan inaendelea kupambana kuhakikisha inainasa saini ya kiungo wa Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa, N’Golo Kante katika dirisha hili la usajili la majira ya kiangazi, na inadaiwa kuwasilisha ofa ya pesa na mchezaji wake Marcelo Brozovic, lakini Chelsea imekataa.

Wababe wa Stanford Bridge wanatajwa kuhitaji zaidi huduma ya Christian Eriksen, aliyewahi kuwika pale Tottenham Hotspur na pesa, ili kumuachia Kante, jambo ambalo Inter Milan haitaki kulisikia kwa kuwa inahitaji kuendelea kupata huduma ya nyota huyo.

Antonio Conte, kocha wa Inter ndiye anayeushawishi zaidi uongozi wa miamba hiyo ya Italia kufanikisha mpango wa kumsainisha Kante, ingawa inaelezwa kwamba kwa sasa timu haina pesa ya kumsajili, hivyo ikiwa inahitajika kuuza baadhi ya wachezaji ili kupata pesa ya kumnunulia.

Vilevile inaelezwa kwamba kitakachomfanya Kante atue Inter Milan ni ushawishi wa Conte aliyewahi kuwa naye pale Chelsea. Ikiwa kocha huyo atafanikiwa kumshawishi ajiunge naye kuna uwezekano mkubwa wa Chelsea ikalazimika tu kumuuza. Kante amekuwa na kiwango bora tangu alipotua Chelsea akitokea Lecester City mwaka 2016, mwaka ambapo pia aliungana na Conte pale Darajani.