Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bakari Msimu afichua jambo

Muktasari:

  • Msimu aliyemaliza na mabao matatu katika ligi hiyo, alisema kupata kwake nafasi kubwa ya kucheza kikosi cha kwanza, hilo limemjengea kujiamini.

KIUNGO mshambuliaji wa Coastal Union, Bakari Selemani Msimu, amesema Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025-2026, ilikuwa bora na imemjenga kiushindani.

Msimu aliyemaliza na mabao matatu katika ligi hiyo, alisema kupata kwake nafasi kubwa ya kucheza kikosi cha kwanza, hilo limemjengea kujiamini.

"Kitendo cha msimu uliomalizika kucheza kwa asilimia kubwa kikosi cha kwanza, kumenifunza nidhamu ya kutunza kiwango, bidii ya mazoezi ya timu na binafsi na ukuaji wa kujua nini nikifanye chenye manufaa kwa timu," alisema na kuongeza;

"Mechi ambazo zimebakia katika kumbukumbu zangu kwa msimu ulioisha ni dhidi ya Prisons tulishinda mabao 4-1, nilifunga bao mojawapo na dhidi ya Singida Black Stars ya Aprili 10, 2025 tulishinda kwa mabao 2-1 nilifunga bao la pili lililoipa pointi tatu timu."

Msimu aliyepandishwa kuichezea timu ya wakubwa 2023-2024 na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera, alisema anatamani kiwango alichokionyesha msimu ulioisha kiwe na muendelezo katika ligi ijayo.

Nyota huyo anayetajwa kusajiliwa Simba kwa ajili ya kuitumikia msimu ujao wa 2026-27, mwenyewe alipoulizwa juu ya taarifa hizo alisema: "Siwezi kujibu swali hilo, Simba ndio inajua wachezaji wake ni kina nani na wao ndio wenye wajibu wa kuwatangaza, jambo la msingi kwangu nilikuwa na msimu mzuri na wenye ushindani wa kunikomaza kiakili."

Mwanaspoti linafahamu kwamba Msimu ameshasaini Simba na dau lake la usajili likiwa ni Sh120 milioni huku mshahara ukitajwa ni Sh6 milioni kwa mwezi.

Katika nafasi anayocheza Msimu, ndani ya kikosi cha Simba kuna Libasse Gueye, Elie Mpanzu na Anicet Oura waliopo kikosi cha kwanza hali ambayo itamfanya afanye kazi ya ziada kama anataka kupata nafasi.