Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzee Pembe aitabiria kichapo Simba

Muktasari:

"Unajua Simba wanajifanya wana pesa ajabu sasa kwenye mechi wanapata matokeo kwa mbinde ndio maana unaambiwa pesa bila maarifa unaweza ukalala sokoni huelewi chakufanya,"amesema.

MSANII mkongwe wa vichekesho nchini, Yusuf Kaimu 'Pembe' amesema kwa namna Simba inavyojiamini nakujiona ina kikosi kipana anaona itaondoka kwa aibu kesho Jumapili Uwanja wa Taifa.
Simba na Yanga inakutana kesho ikiwa ni mechi ya mzunguko wa pili baada ya raundi ya kwanza kutoka sare ya mabao 2-2, Wanamsimbazi wakiwa ndio wenyeji wa mchezo.
Pembe  hajifichi kwamba ni Yanga lialia amesema mashabiki wa Simba wajengwe kisaikolojia ili wakifungwa wasiwe wanavunja viti.
"Yanga ni wazalendo ndio maana ikitokea tukifungwa tunaondoka nyumbani kwa ustaarabu, Simba sasa wanang'oa viti, makabati, meza na ndio wakorofi mtaani,"
"Unajua Simba wanajifanya wana pesa ajabu sasa kwenye mechi wanapata matokeo kwa mbinde ndio maana unaambiwa pesa bila maarifa unaweza ukalala sokoni huelewi chakufanya,"amesema.
MORRISON KIZIZI CHA YANGA
Kila kona unakopita mashabiki wa Yanga lazima wataje jina la winga wao, Bernard Morrison kwamba atawakarahisha Simba akitembea juu ya mpira.
Pembe amesema Morrison ni mchezaji anayemvutia nakuona atafanya maajabu katika mechi hiyo na kwamba ndiye atakayewafunga midomo Simba.
"Naikubali timu yote lakini Morrison ananivutia zaidi kutokana na ujuzi wake anafanya soka liwe rahisi, hivyo siwapatii picha hao upande wa pili watakavyokuwa wanamtolea macho wanatamani angekuwa mchezaji wao,"amesema.

Imeandaliwa na Olipa Assa, Oliver Albert na Doris Maliyaga