Mzamiru aivunja kambi ya makapera Simba achukua jiko jumla

Muktasari:
Kukosa muda wa kupumzika, usafi wa nguo hasa za mazoezi lakini ukiwa ndani ya ndoa vitu hivi kwa asilimia kubwa unasaidiwa na mkeo
Dar es Salaam. NI miezi kumi na moja sasa tangu Kiungo wa Simba, Mzamiru Yassin afunge ndoa Septemba 2 mwaka jana.
Mzamiru, ambaye alijiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar alifunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu baada ya kufikia makubaliano ya kuishi pamoja na kuanzisha familia.
Watu wengi wanaamini mchezaji akiingia kwenye ndoa kiwango chake kinashuka kwa hili Mzamiru anasema:
“Sio kweli na kubainisha tangu ameingia kwenye ndoa kiwango chake kimeimarika kutokana na mambo mengi niliyokuwa nafanya mwenyewe sasa nafanyiwa na mke wangu.
MBONA KUOA MZUKA
“Hakuna maisha mazuri kama kucheza mpira ukiwa kwenye ndoa kwani, kwa upande wangu na naamini hata wachezaji wasiooa wanapitia hili kuumiza kichwa juu ya kula chakula gani hasa wakitoka mazoezini.
“Kukosa muda wa kupumzika, usafi wa nguo hasa za mazoezi lakini ukiwa ndani ya ndoa vitu hivi kwa asilimia kubwa unasaidiwa na mkeo.”
HUMWAMBII KITU KWA MWINYI, NDITI
Kila mwanadamu huwa anakuwa wa mtu, ambaye anatamani kuwa kuwa kama mtu fulani kwa kupenda kile anachokifanya. Kwa upande wa Mzamiru anabainisha kuwa nyota waliomvutia kuingia katika soka ni Mwinyi Kazimoto na Shabani Nditi kwa kuweka wazi kuwa na ndio wachezaji anaowkubali kwa soka la kibongo.
“Kazimoto na Nditi ni wachezaji wa muda mrefu naweza kusema ni miongoni mwa nyota wanaojitunza na ndio maana wameweza kudumu katika soka muda mrefu huku viwango vyao vikiendelea kuimarika.
“Napenda wanavyocheza japo kila mmoja anasifa zake awapo dimbani na mpira ninachoweza weza kusema ni kwamba, wanajua wanachokifanya na wanaheshimu kazi.
“Ni wachezaji wa kuigwa na chipukizi ikiwa ni sambamba na nyota wengine ambao, hawaheshimu soka na kuchukulia kama mchezo wa kihuni,” anasema Mzamiru.
AMETIMIZA NDOTO YAKE
Kila mtu ana mipango yake tangu anaanza kujitambua anakuwa na mipango ya kufanya akiwa amefikisha umri wa kujisimamia mwenyewe.
Mzamiru anabainisha kuwa tangu akiwa na umri mdogo alikuwa anapenda