Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwenyekiti Mkoa wa Iringa awapa Mkwawa Queens 2 milioni

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Daudi Yassin Akikabidhi Kitita cha sh 2 Milioni Kwa uongozi wa Timu ya wanawake Mkwawa Queens ( Picha na Mary Sanyiwa, Iringa)

Muktasari:

  • Akikabidhi msaada huo jana kwa uongozi wa timu hiyo, Yassin amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kinatambua mchango mkubwa wa timu hiyo pamoja na timu nyingine katika mchezo huo.

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Iringa, Daud Yassin amekabidhi kitita Cha sh 2 Milioni kwa uongozi wa timu ya Mkwawa Queens inayocheza Ligi Kuu ya Wanawake, ambayo inayotarajia kusafiri Jumapili kwenda Dar es Salaam kucheza dhidi Simba Queens.

Akikabidhi msaada huo jana kwa uongozi wa timu hiyo, Yassin amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kinatambua mchango mkubwa wa timu hiyo pamoja na timu nyingine katika mchezo huo.

Aidha mwenyekiti huyo amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekuwa akiendeleza michezo hapa nchini hivyo wao kama CCM Mkoa wataendelea kuunga mkono jitihada hizo sanjari na kusaidia  Sekta ya michezo mkoani hapa

"Tunaona jitihada za Mkwawa Queens timu yetu inatimiza vema majukumu yake ni vema wadau kuendelea kuziunga mkono timu zote ndani ya mkoa wetu lakini pia niwapongeze uongozi wa Mkwawa Queens kwa kuendelea kuwakilisha mkoa wetu vizuri katika soka hili la Wanawake." Amesema.

Kwa upande wake Afisa habari wa timu hiyo, Francis Godwin ameshukuru mchango ambao umetolewa na mwenyekiti huyo huku akisema kwamba zaidi ya sh 10 Milioni bado zinahitajika ili kukamilisha  mzunguko uliobaki.

"Kwa sasa timu yetu inatarajia kwenda Dar es Salaam kucheza na Simba Queens siku ya Jumanne, hivyo tutaondoka Iringa Jumapili Aprili 16, lakini safari hiyo itagharimu sh 3.4 Milioni huku tukijiandaa na mchezo wa Dodoma pamoja na Lindi ambapo sh 10 Milioni bado zinahitajika kukamilisha mizunguko hiyo." Amesema Godwin

Hata hivyo, Godwin amewataja wadau wengine ambao wamechangia kuwa ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Iringa Ritta Kabati ambapo amechangia sh 200,000 pamoja na wadau wengine ambao wanaendelea kujitolea akiwemo Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini Jackson Mnyawami.