Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwaterema: Acheni utani, ligi msimu huu ngumu

MSHAMBULIAJI wa Kagera Sugar, Hassan Mwaterema amesema ushindani katika Ligi Kuu Bara msimu umekuwa ni mkubwa tofauti na misimu ya nyuma.

Akizungunmza na Mwanaspoti, Mwaterema alisema siri kubwa ni uwekezaji uliopo unaozipa timu kiburi cha kusajili nyota wakali kwa ajili ya kuzisaidia kwenye michuano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

“Mechi zimesalia nne ila hadi sasa ukiangalia ushindani mkubwa upo kwenye (timu) zinazowania kusalia msimu ujao, lakini pia hata zile timu za kumaliza nafasi ya tatu na nne bado ni ngumu kubashiri,” alisema.

“Kufunga ni nafasi na huwezi kufanya hivyo kwenye kila mchezo kwani ninachozingatia kwangu ni kuona timu yetu inapiga hatua kwani nafasi tuliyopo inatupa motisha ya kupambana ili tumalize hata nafasi nne za juu.”

Nyota huyo mwenye mabao matatu katika kikosi hicho, msimu huu ameandamwa na jinamizi la kutofunga hivi karibuni kwani mchezo wake wa mwisho kutupia nyavuni ulikuwa ni dhidi ya Mbeya City Machi 12, kwenye ushindi wa timu hiyo wa bao 1-0.