Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwamuzi mechi ya Simba, Mashujaa FC achunguzwa

Muktasari:

  • Akizungumzia uwepo wa taarifa za mmoja wa waamuzi wasaidizi aliyekuwa sehemu ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Mashujaa uliochezwa juzi, Ijumaa, kudaiwa kuwa ni mwanachama wa klabu mojawapo kati ya hizo, bosi huyo wa waamuzi alisema kama chama hawana hizo taarifa.

MWENYEKITI wa Kamati ya Waamuzi Tanzania, Nassor Hamduni amesema kwa mujibu wa kanuni za Chama cha Waamuzi Tanzania (FRAT), hairuhusiwi mwamuzi kuwa mwanachama wa klabu na kama ikibainika atafutwa kazi.

Akizungumzia uwepo wa taarifa za mmoja wa waamuzi wasaidizi aliyekuwa sehemu ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Mashujaa uliochezwa jana, Ijumaa, kudaiwa kuwa ni mwanachama wa klabu mojawapo kati ya hizo, bosi huyo wa waamuzi alisema kama chama hawana hizo taarifa.

“Hatuna taarifa za (anamtaja jina) kuwa mwanachama na kama tukipata ushahidi uliojitosheleza, basi hatuna budi kumuacha akaendelea na majukumu yake kwenye klabu yake kwa sababu sheria hairuhusu kuwa na mwanachama wa timu fulani kisha akachezesha mpira,” alisema na kuongeza:

“Kama ninyi waandishi au wadau wa mpira kuna mtu ambaye ana ushahidi unaotosheleza kututhibitishia kuwa ni mwanachama tunaomba mtusaidie ili kuweka mambo sawa na kuzingatia kanuni na sheria zetu kutoruhusu mwamuzi kuwa mwanachama.”

Hata hivyo, gazeti hili halikumpata mwamuzi husika kuzungumzia madai hayo.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, Simba ilitoka nyuma na kupata ushindi wa mabao 2-1 ikifikisha pointi 60 na kuendelea kusalia katika nafasi ya pili kwenye msimamo.

Mbali na hilo, Hamduni alitolea ufafanuzi muda ulioongezwa katika mchezo huo, akisema hawezi kuingilia uamuzi wa mwamuzi kwani ndiye anayefahamu uliopotea na unatakiwa kufidiwa vipi.

“Ni haki yake ya msingi mwamuzi kuongeza muda. Hakuna sheria ambayo inatufunga tumpangie muda wa kuongeza, nafikiri kwenye suala hilo sina sababu ya kuzungumzia zaidi, alikuwa sahihi,” alisema.

Katika mchezo huo, kipindi cha kwanza baada ya dakika 45 kutimia ziliongezwa dakika sita huku mwamuzi wa kati Kefa Kayombo akipuliza kipenga kuashiria mapumziko baada ya dakika ya tisa na kufanya mechi kuchezwa kwa dakika tatu zaidi.

Kipindi cha pili ziliongezwa dakika 15, huku filimbi ya mwisho ikipulizwa dakika ya 19, ikiwa ni nyongeza ya dakika nne zaidi ya zile zilizoongezwa.

Hata hivyo, katika mchezo huo kulikuwa na matukio kadhaa yaliyosababisha mchezo kusimama ikiwamo kadi ya pili ya njano aliyoonyeshwa kipa wa Mashujaa, Patrick Munthari katika dakika ya 80 iliyofuatiwa nakadi nyekundu. Pia matukio ya ‘sub’ za wachezaji na penalti mbili zilizopigwa na Simba katika dakika za 65 na 90+19.