Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mushi mzuka mwingi ufungaji pointi kikapu

MUSHI Pict

Muktasari:

  • Mushi aliyewahi kuwa mfungaji bora katika mashindano ya kanda ya tano ya Afrika, ameshika nafasi hiyo baada ya kufunga pointi 128.

BAADA ya Jonas Mushi kutoka timu ya Stein Warriors kushika nafasi sita katika ufungaji wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), ametamba kurudi katika nafasi yake ya kwanza aliyoizoea.

Mushi aliyewahi kuwa mfungaji bora katika mashindano ya kanda ya tano ya Afrika, ameshika nafasi hiyo baada ya kufunga pointi 128.

Kwa mujibu wa Mushi, imekuwa ni kawaida kwake, kushika nafasi ya kwanza baada ya Ligi kumalizika. 

“Pointi 85 nilizozidiwa na  Ntibonela Bukeng wa timu ya Savio kwa upande wangu   naona ni pointi chache,” alisema Mushi.

 Katika msimamo wa ufungaji, nyota huyo wa Savio anaongoza kwa kufunga pointi 213, akifuatiwa na mchezaji mwen-zake Godfrey Swai aliyefunga pointi 159.

Wakati huo huo, Mushi anashika nafasi ya 7 ya ufungaji wa eneo moja la three pointi 17,  huku Ally Abdallah wa timu ya Dar City akishika nafasi ya kwanza kwa kufunga 20.

Wakati Ligi ya kikapu BDL ikitarajiwa kuanza Julai 10, imeonyesha mchuano mkali huko kwa upande wa udakaji wa mipi-ra (rebound), kwa wachezaji.

 Wachezaji hao ni Victor Michael kutoka Vijana “City Bulls” aliyeongoza kwa kudaka mara 80, akifuatiwa na Daniel Mi-chael aliyedaka mara 76, Elias Nshishi (ABC) 76, Junior Louisisi (Srelio) 68 na Aloyce Boniphace (Mchenga Star) 66.