Mukoko aiokoa Yanga, Feisal amwaga machozi

Yanga imepata sare nyingine lakini safari hii wakiwa nyumbani baada ya kufungana na Kagera Sugar kwa mabao 3-3.
Aliyewaumiza Yanga alikuwa ni kiungo Mukoko Tonombe ambaye alianzia benchi huku nafasi yake akianza Zawadi Mauya kisha timu yake kuonekana kuzidiwa katika dakika 45 za kwanza.
Hata hivyo alikuwa ni Mukoko ndiye aliwafichia aibu Yanga baada kuingia kipindi cha pili akifunga bao ambalo lilioipa timu yake alama moja baada ya bao lake la.dakika ya 60 kwa shuti kali.
Yanga ndio waliouanza mchezo kwa kasi dakika ya tatu tu walitengeneza shambulizi kali wakipiga pasi za haraka kisha mpira kumkuta winga Tuisila Kisinda lakini krosi yake nzuri Farid Mussa anashindwa kuitumia kufunga inakuwa ndefu.

Dakika ya 5 kipa Kagera Sugar Said Kipao anafanya kazi nzuri kutoka katika eneo lake la hatari na kuuwahi mpira akiokoa shambulizi zuri la Yanga wakati Michael Sarpong akiiwahi pasi safi ya kupenyezwa iliyopigwa na kiungo Deuse Kaseke.
Dakika ya 11 Kagera walifanikiwa kupata bao likifungwa na kiungo Peter Mwalyanzi akimalizia krosi safi ya beki wa kulia Mwaita Geleza wakati wageni wakitengeneza shambulizi zuri.
Bao hilo hata hivyo lilidumu kwa dakika mbili pekee pekee ambapo dakika ya Yanga dakika ya 12 walifanikiwa kupata penalti iliyotokana na shuti Kisinda baada ya beki mmoja wa Kagera kuunawa mpira wakati akitaka kuokoa.
Penalti hiyo ilipigwa na Kisinda ambaye aliuweka mpira wavuni ingawa Kipao aliugusa kidogo wakati ukielekea wavuni.
Yanga walifanya shambulizi lingine zuri dakika ya 18 Sarpong anashindwa kufunga kwa akiwa karibu na uso na Kipawa shuti lake linadakwa vyema akipokea pasi ya Kaseke.
Kagera walioonekana kutulia walifanikiwa kurudi katika kuongoza tena kupitia bao safi la Hassa Mwaterema aliyeunasa mpira mrefu wa beki wake David Luhende kisha kukimbia nao ndani ya eneo la hatari akawatingisha mabeki wa Yanga kisha kuachia shuti kali lililojaa wavuni.
Wakati wote Yanga ilionekana kuzidiwa katikati ya kiungo hasa eneo la kiungo
almanusura Kagera wapate bao tatu dakika ya 25 Nassoro Kapama anapoteza nafasi ya wazi kipa Metacha Mnata anapangua shuti lake wakati mabeki wa Yanga wakijichanganya na mpigaji kuunasa mpira.
Hata hivyo dakika ya 29 Kaseke alifanikiwa kuisawazishia Yanga akimalizia kwa uzuri pasi ya Sarpong wakati Yanga wakitulia na kutengeneza shambulizi zuri.
Wakati Yanga wakidhani watakwenda mapumziko kwa sare hiyo walijikuta wakiruhusu bao la tatu kwa makosa yaleyale ya safu ya ulinzi kwa bao lililofungwa na mshambuliaji wao wa zamani Yusuf Mhilu akifunga kwa kichwa safi akipokea mpira wa kona fupi uliopigwa na Luhende.
Mpaka mapumziko Yanga ilitoka ikiwa kichwa chini kwa mabao 2-3 huku mashabiki wao wakionekana kuchukizwa na jinsi timu yao ilivyocheza kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Yanga ilirudi na kufanya mabadiliko mawili wakimtoa Mauya nafasi yake ikichukuliwa na Mukoko Tonombe lakini pia akitolewa Sarpong nafasi yake ilichukuliwa na Ditram Nchimbi.
Mabadiliko hayo yalionekana kuipa nguvu Yanga na kuonekana kutulia na kutawala mchezo wakiishambulia muda wote wageni wao.
Alikuwa Tonombe dakika ya 60 akiisawazishia Yanga kwa bao safi la shuti kali la nje ya eneo la 18 na kujaa moja kwa Moja wavuni akipokea pasi ya Nchimbi.
Yanga waliendelea kuliandama lango la Kagera lakini utulivu wa kumalizia.
Yanga watajilaumu kwa nafasi waliyoipata dakika ya 87 wakati Feisal Salum alipokimbia na mpira mrefu lakini akiwa USO na kipa Kipao anatoa pasi kwa Nchimbi lakini akaipoteza
Feisal aangua kilio
Matokeo hayo yalibaki hivyo mpaka mwisho wa mchezo ambapo nafasi hiyo yw Feisal ilionekana kumuumiza akiangua kilio mara baada ya firimbi ya mwisho huku wachezaji wenzake wakionekana kumfariji.
Yanga
Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha ,Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Zawadi Mauya/Tonombe, Feisal Salum, Tuisila Kisinda, Farid Mussa, Michael Sarpong/Ditram Nchimbi, Deuse Kaseke/Haruna Niyonzima.
Kagera Sugar
Said Kipao, Mwaita Gereza, David Luhende, Hassan Isihaka/Yusuf Mlipili, Abdallah Mfuko, Abdulswamad Kassim, Yusuf Mhilu, Abdallah Seseme/Mohamed ibrahim, Nassoro Kapama, Peter Mwalyanzi/Ally Nassoro