Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtibwa pointi, Namungo nafasi,

Muktasari:

  • Namungo imecheza mechi 27, imeshinda  saba sare 10 na imefungwa  10, inamiliki mabao 22, imefungwa mabao 25 na imekusanya pointi 3, ipo nafasi ya nane,  wakati Mtibwa ipo mkiani kwa pointi 20, katika mechi 27 iliyocheza imeshinda tano, sare tano, imefungwa 17, inamiliki mabao 27, imefungwa mabao 46.

MECHI ya Mei 20, itakayopigwa Uwanja wa Namungo, Morogoro, itakuwa ya kusaka nafasi kwa Namungo kupanda nafasi za juu kwa  Mtibwa Sugar kuongeza pointi hata ikishinda itasalia nafasi ileile (mkiani).

Namungo imecheza mechi 27, imeshinda  saba sare 10 na imefungwa  10, inamiliki mabao 22, imefungwa mabao 25 na imekusanya pointi 3, ipo nafasi ya nane,  wakati Mtibwa ipo mkiani kwa pointi 20, katika mechi 27 iliyocheza imeshinda tano, sare tano, imefungwa 17, inamiliki mabao 27, imefungwa mabao 46.

Mzunguko wa kwanza mechi iliyopigwa Desemba 7, Uwanja Majaliwa uliopo Ruangwa mkoani Lindi, Namung1-0 Mtibwa Sugar.


WACHEZAJI WAZOEFU

Timu hizo zina wachezaji wazoefu wanaoweza kumua mechi hiyo kwa upande wa Namungo FC baadhi ya ni Erasto Nyoni, Meddie Kagere, Jacob Masawe na Pius Buswita.    

Kwa Mtibwa,  washambuliaji ni Charles Ilanfya, Rashid Juma, makipa Mohamed Mkaka na wa kigeni Justin Ndikumana, beki Oscar Masai, hivyo hautakuwa mchezo rahisi licha ya timu hiyo, kuburuzwa mkiani.


MISIMU MINNE NYUMA 2022/23

Namungo 2-2 Mtibwa Sugar  (Agosti 15)

Mtibwa Sugar 1-1 Namungo FC (Desemba 16) 2021/22 

Namungo 3-1 Mtibwa Sugar (Feb 6)

Mtibwa Sugar 2-4 Namungo (Juni 26) 2020/21

Mtibwa Sugar 1-0 Namungo FC (Oktoba 7)

Namungo 1-0 Mtibwa Sugar (Mei 12) 2019/20

Namungo 1-0 Mtibwa Sugar (Oktoba 23)

Mtibwa Sugar 1-1 Namungo (Mei 4).


MAKOCHA/WADAU

Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila  amesema "Kushika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu, hakumanishi ndio mwisho wa kupambana kwetu, tunachotakiwa ni kushinda mechi zote, Namungo ina wachezaji wazoefu tutapambana nao.

Kwa upande wa  kocha mkuu wa Namungo FC, Mwinyi Zahera amesema "Tunahitaji kupanda nafasi za juu, najua mchezo hautakuwa rahisi, ila wachezaji wangu wapo tayari kupambania pointi tatu, kutoka kwa Mtibwa.

Mshambuliaji wa zamani wa Mtibwa Sugar, Abdallah Juma ambaye aliwahi kuibuka mfungaji bora mara mbili (2003 na 2006), asema "Kiukweli Mtibwa ipo wakati mgumu, ingawa huo mchezo utakuwa mgumu, dakika 90 ndizo zitakazoamua.