Mtanzania asaini minne kucheza Serbia
Aliyekuwa nahodha wa timu ya Taifa chini ya miaka 17 katika michuano ya ya Mataifa Afrika Morice Abraham amesaini mkataba wa miaka 4 na klabu ya FK Spartak Subotica inayoshiriki Ligi Kuu ya Serbia
Akizungumza na Mwanaspoti Morice Abraham amethibitisha kusaini na timU hiyo baada ya vuta ni kuvute ya muda mrefu kati yake na timu ya Alliance ya Mwanza
“Ni kweli nimesaini kandarasi ya miaka minne kuitumikia klablu yangu mpya ya FK Spartak Subortika baada ya miezi 3 ya kuwa huku kwenye majaribio na jana nimecheza mchezo wangu wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Backa Topola uliomalizika kwa sare ya 0-0” alisema Morice
Pia Morice amemshukuru nahodha wa Taifa Stars Bwana Samata pamoja na tasisi yake ya kusimamia wachezaji ya Samaplayer managment kwa kumsaidia kufika hapa.
“Namshukuru sana nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samata kwani kupitia taasisi yake alinikuta nyumbani Tabata akanishika mkono na kunisaidia kufika hapa” alisema Morice