Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtambuka aamsha morali Songea United

Mtambuka Pict

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Mingange alisema usajili wa mchezaji huyo utaongeza chachu ya ushindani ndani ya kikosi hicho katika kutimiza malengo ya kukipandisha Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao, huku akiweka wazi anatambua vyema kipaji chake.

KLABU ya Songea United ya mkoani Ruvuma imekamilisha usajili wa aliyekuwa mshambuliaji wa TMA ya jijini Arusha, Abiud Mtambuka kwa mkataba wa miezi sita, huku kocha wa kikosi hicho, Meja Mstaafu, Abdul Mingange akijivunia usajili wake.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mingange alisema usajili wa mchezaji huyo utaongeza chachu ya ushindani ndani ya kikosi hicho katika kutimiza malengo ya kukipandisha Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao, huku akiweka wazi anatambua vyema kipaji chake.

“Nilishawahi kufanya naye kazi nikiwa Mashujaa hivyo namtambua vizuri, ni mchezaji mzuri na naamini ataongeza morali na ushindani kwa washambuliaji wengine waliopo hapa, bado tunaendelea na mikakati ya kuboresha maeneo mbalimbali,” alisema.

Kocha huyo wa zamani wa Ndanda FC, Mbeya City na Tanzania Prisons aliyejiunga na Songea United akitokea Stand United ya mkoani Shinyanga, aliongeza hawako nafasi mbaya sana ingawa wanapaswa kujipanga zaidi.