Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo waanza kuwasili Bodi ya Ligi kujadili dabi

Muktasari:

  • Mkutano huo unaofanyika asubuhi hii kwenye ofisi za TPLB zilizopo Ilala, jijini Dar es Salaam ambapo viongozi wameanza kufika wakitanguliwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo, Almas Kasongo aliyefika saa 2:37 asubuhi.

Mkutano wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) na viongozi wa Yanga umeanza kuwakusanya vigogo mbalimbali wakianza kuwasili eneo la tukio.

Mkutano huo unaofanyika asubuhi hii kwenye ofisi za TPLB zilizopo Ilala, jijini Dar es Salaam ambapo viongozi wameanza kufika wakitanguliwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo, Almas Kasongo aliyefika saa 2:37 asubuhi.

Baada ya Kasongo alifuata Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Nassoro Idrissa 'Father' ambaye pia ni Mwenyekiti wa Azam FC, kisha akafuata Mwenyekiti wake Steven Mnguto na Heri Misinga ambaye ni Mjumbe wa Bodi na Mwenyekiti wa KMC.

Viongozi wa Yanga bado hawajaaanza kuwasili na Mwanaspoti linafahamu kwamba viongozi hao watafika wakiongozwa na Makamu wa Rais, Arafat Haji na wajumbe wengine wa Kamati ya Utendaji.

Hali ya mazingira nje ya ofisi hizo, ipo tulivu hakuna bughudha zaidi ya ulinzi mkali ambao unawazuia waandishi wa habari kuingia ndani ya jengo hilo.