Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Viongozi Yanga watua Bodi ya Ligi na wanasheria

Muktasari:

  • Msafara wa Yanga umefika saa 4:12 asubuhi ikiongozwa na Makamu wa Rais, Arafat Haji na wajumbe wa Kamati ya Utendaji Alexander Ngai, Rodgers Gumbo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano.

Yanga imefika rasmi katika kikao chao na Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), huku msafara wa timu hiyo ukiwahusisha viongozi watano na wanasheria watatu.

Msafara wa Yanga umefika saa 4:12 asubuhi ikiongozwa na Makamu wa Rais, Arafat Haji na wajumbe wa Kamati ya Utendaji Alexander Ngai, Rodgers Gumbo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano.

Wengine ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu, Andre Mtine, Ofisa Habari wa timu hiyo Ally Kamwe na wanasheria watatu tayari kwa kikao hicho cha kujadili Dabi ya Kariakoo.

Mara baada ya kuwasili Arafat amesema kwa kifupi kwamba:"Tumefika na muungwana hakatai wito," amesema kwa kifupi Arafat wakati aliingia ndani ya ofisi za Bodi hiyo.