Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtaijua Yanga, yagaragaza maafande Dar

Mrisho Ngassa akishangilia baada ya kufunga bao katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baina ya Yanga na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana Ijumaa. Picha na Michael Matemanga

Muktasari:

  • Simba ilikalia usukani wa ligi hiyo kwa kipindi kirefu baada ya kuiporomosha JKT Ruvu. Hiyo ni mechi ya tano mfululizo JKT Ruvu inapoteza chini ya kocha, Mbwana Makatta. Awali ilipoteza mbele ya Mtibwa, Azam, Mbeya City na Rhino

 

 

YANGA imeipiga JKT Ruvu mabao 4-0 na kukalia usukani wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kufikisha pointi 25. Kwa matokeo hayo benchi la ufundi pamoja na wachezaji wake wamepata kiburi cha aina yake na kusema: “Sasa ndiyo mtaijua Yanga”

Simba ilikalia usukani wa ligi hiyo kwa kipindi kirefu baada ya kuiporomosha JKT Ruvu. Hiyo ni mechi ya tano mfululizo JKT Ruvu inapoteza chini ya kocha, Mbwana Makatta. Awali ilipoteza mbele ya Mtibwa, Azam, Mbeya City na Rhino.

Kwa matokeo hayo ya jana Ijumaa, Yanga imezishusha kileleni Azam na Mbeya City zilizokuwa zimeshikilia nafasi mbili za juu kwa pointi 23 kila moja.

Lakini raha ya Yanga kukaa kileleni inaweza kuharibika leo Jumamosi kwani Azam inacheza na Ruvu Shooting kwenye uwanja wake wa Chamanzi na ikishinda itafikisha pointi 26.

Hata kama mambo yasipoiendea vizuri Azam, Mbeya City itacheza kesho Jumapili jijini Mbeya dhidi ya timu laini Ashanti United. Lakini Yanga imedai haitishwi na timu hizo mbili.

Walioimaliza JKT Ruvu, ni Mrisho Ngassa aliyefunga mawili, Oscar Joshua na Jerry Tegete.

Ngassa alitumia dakika tatu tu uwanjani tangu mpira uanze akapiga shuti la mbali nje ya boksi lililoandika bao la kwanza. Dakika ya 12 akafunga jingine kwa kichwa akiwa katikati ya mabeki watatu akiunganisha mpira wa kurushwa wa Mbuyu Twite.

Oscar Joshua ambaye katika siku za karibu amekuwa hana uhakika wa namba kwenye kikosi cha kwanza, alipiga bao la tatu dakika ya 46 kwa shuti kali pembeni lililokwenda moja kwa moja langoni mwa JKT na hapo ndipo macho ya kocha wa Wanajeshi yakabadilika rangi na kuwa mekundu.

Jerry Tegete ambaye amekuwa akikalia benchi kumpisha Mrundi Didier Kavumbagu, aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mrundi huyo na dakika ya 88 swahiba yake mkubwa, Ngassa akampa bonge la krosi, naye akapiga bao la nne.

Kipindi cha kwanza JKT ilionekana kuchanganyana na kushindwa kuihimili Yanga kwenye idara zote ingawa Amos Mgisa alipenya mara kadhaa kwenye ulinzi wa Yanga, lakini akashindwa kufanya kitu cha maana.

Amos Mgisa na Haruna Adolf walipiga mashuti kadhaa kwa nyakati tofauti kwenye lango la Yanga, lakini kipa Deo Munishi ‘Dida’ akapangua kilaini na kuiacha JKT Ruvu iking’ang’ania nafasi ya tisa na pointi zake 12.

Kocha wa Yanga, Ernest Brandts, alisema mechi ilikuwa ngumu na wapinzani wake walikuwa wakibutua mara kadhaa, lakini akatupia lawama kwa washambuliaji wake ambao walikosa mabao mengi ya wazi.

Lakini amesisitiza akisema: “Tumeingia kwenye nafasi nzuri na mapambano yanaendelea.”

Makata wa JKT alilalamika: “Tumefungwa kwa sababu ya uchovu, timu imewasili saa nane usiku (kuamkia jana Ijumaa) ikitokea Tabora, njiani gari liliharibika. Tuliomba mechi isogezwe mbele wakatukatalia kabisa.”

Ngassa aliiambia Mwanaspoti kuwa mabao mawili aliyofunga ni zawadi kwa straika, Paul Ndauka, ambaye kabla ya mchezo huo alimtabiria atamfunga idadi hiyo ya mabao.

Yanga; Deogratius Munishi, Mbuyu Twite/Ibrahim Job, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Kelvin Yondani/Reliants Lusajo, Athuman Idd, Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu/Jerry Tegete, Mrisho Ngassa na Hamis Kiiza.

JKT Ruvu; Sadik Mecks, Musa Zubeiry, Kessy Mapande, Omary Mtaki, Damas Makwaiya, Nashom Naftar, Amos Mgisa, Haruna Adolf, Paul Ndauka, Samuel Kamutu, Sostenes Manyasi.

Leo Jumamosi ni Mambo Shooting vs Coastal, Prisons na Oljoro huku Mtibwa ikipambana na Rhino Rangers.