Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dube azua hofu kambi ya Yanga fainali FA

Muktasari:

  • Dube aliyefunga mabao 13 katika Ligi Kuu Bara na mawili Kombe la FA, alipata majeraha ya nyama za paja Yanga ilipovaana na Tanzania Prisons uliochezwa Juni 18, 2025.

LICHA ya kucheza mechi iliyopita ya Ligi dhidi ya Simba, lakini taarifa kutoka katika kambi ya Yanga zinabainisha mshambuliaji huyo hali yake sio nzuri.

Dube aliyefunga mabao 13 katika Ligi Kuu Bara na mawili Kombe la FA, alipata majeraha ya nyama za paja Yanga ilipovaana na Tanzania Prisons uliochezwa Juni 18, 2025.

Majeraha hayo yalimfanya kuikosa mechi iliyofuata dhidi ya Dodoma Jiji iliyochezwa Juni 22, 2025 hali iliyoibua huenda angeikosa Dabi ya Kariakoo, lakini akaibukia kikosi cha kwanza na kucheza kwa dakika 45 kabla ya kumpisha Clement Mzize.

Sasa basi, Yanga ikijiandaa kuvaana na Singida Black Stars katika mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho (FA), mshambuliaji yupo katika hatihati ya kucheza.

Kocha wa Yanga, Miloud Hamdi, amesema mbali na Dube, wachezaji wengine wote wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo.

"Hadi sasa sina uhakika kama tutamkosa mchezaji yeyote, lakini kutokana na kucheza mechi nne ndani ya siku 10 inawezekana hali hiyo ikawepo kwa sababu wanaweza kupoteza nguvu.

"Nina mchezaji mmoja ambaye naamini kesho sijui itakuwaje, ni Dube. Wengine wote wapo sawa.

"Dube pekee ndiye ana shaka ya kuwepo kwa sababu, jana wakati wa mazoezi alisema hajisikii vizuri lakini kesho tutaona hali yake itakuwaje," amesema Hamdi.

Straika huyo raia wa Zimbabwe alijiunga na Yanga msimu huu akitokea Azam FC aliyoitumikia kwa misimu minne tangu 2020 aliposajiliwa kutoka Highlanders ya Zimbabwe na ameifungia mabao 13 na asisti tisa katika Ligi Kuu hadi sasa.

Kombinesheni yake na Mzize, Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli imezalisha jumla ya mabao 40 kati ya 83 iliyofunga timu msimu huu ikitetea taji la Ligi Kuu kwa msimu wa nne mfululizo.