Msuva azikwepa Simba, Yanga
Mabingwa wa Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika Al Ahly (Misri), Es Tunis (Tunisia) na Wydad Casablanca (Morocco) ndio timu tatu pekee ambazo Barani Afrika ambazo hazitaanzia katika hatua ya awali kwenye Ligi ya Mabingwa inayotarajiwa kuanza Septemba mwaka huu.
Wydad ambao ni mabingwa wa kombe la Ligi kuu nchini Morocco itaongozwa na Mtanzania Simon Msuva ambaye anakipiga katika klabu hiyo na kutokana na timu hiyo kutoanzia kwenye hatua ya awali ni wazi atazikwepa timu za Tanzania Simba na Yanga katika hatua hiyo
Kaizer Chief ambao waliingia Fainali na Al Ahly kisha kupoteza kwa mabao 3-0 wamekosa nafasi hiyo baada ya kumaliza nafasi ya nane kwenye Ligi yao ya Afrika Kusini na kukosa sifa ya kucheza kimataifa.
Simba na Yanga ndio timu pekee zinazoiwakilisha Tanzania katika michuano hiyo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika huku Azam FC na Biashara United zikiiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
IMEANDIKWA NA DAUDI ELIBAHATI