Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msuva awatangazia vita Kaizer Chief

KUMEKUCHA!! Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva anayekipiga huko Morocco akiwa na Wydad Casablanca, amewatangazia vita Kaizer Chief ya Afrika Kusini kwa kusema lazima kitaeleweka hiyo, Jumamosi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika inatarajiwa kuanza kutimua vimbi wikiendi ijayo, wakati Simba wakianzia DR Congo kuikabili AS Vita, Wydad Casablanca anayoichezea Msuva itakuwa nyumbani kuikaribisha Kaizer Chief.

Kwa maandalizi ambayo walikuwa wakiyafanya wakati Ligi yao ya ndani ikiwa imesimama kutokana na ushiriki wa Morocco kwenye mashindano ya Chan, Msuva anaamini yamewajenga na wanaweza kuwasapraizi vilivyo wapinzani wao. “Tumekuwa na kipindi kizuri cha maandalizi ni wachezaji wetu wachache walienda Cameroon kwa ajili ya mashindano ya Chan hivyo asilimia kubwa tulikuwa tukiendelea na mandalizi, niliendelea kuwasoma wenzangu na kujifunza mambo ya ziada ambayo yanaweza kutusaidia kama timu,”

“Binafasi nilijipa kazi ya kuwasoma wapinzani wetu kwa kuangia baadhi ya mechi zao ili kuona ni aina gani ya mabeki ambao naenda kukabiliana nao, nadhani hii itanisaidia kwa sababu najua umuhimu wa haya mashindano kwangu, nahitaji kuonyesha uwezo nilionao,” alisema na kuongeza. “Mchezaji mkubwa huonekana kwenye michezo mikubwa, aina hii ya mechi ndizo ambazo nilikuwa nikiziota na kwa ukubwa wa timu niliyopo naamini nitaonekana kwa sababu kuwa hapa ni fursa kwangu nahitaji kusonga mbele bado,” alisema.

Akiongelea kiwango cha Kaizer kwenye, alisema sio nzuri sana lakini hilo halijawafanya kuwachukulia poa na kuweka akilini mwao kuwa wanaenda kukutana na timu dhaifu na badala yake mkazo umekuwa mkubwa.

“Hakuna timu dhaifu kwenye Ligi ya Mabingwa, hata kama mwenendo wao sio mzuri kwenye ligi, wanaweza kuwa hatari na wakatudhuru kama tukisema tuwachukulia kwa mtazamo huo.