Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msuva aiokoa Stars na kichapo

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Sudan katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa uliomalizika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Katika mchezo huo ulio kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Stars kwenda mapumziko kikiongozwa bao 1-0 lililofungwa na Toto Siddig katika dakika ya pili ya mchezo.

Kipindi cha pili kilianza kwa Stars kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Zawadi Mauya, Ibrahim Joshua na Kelvin John huku nafasi zao zikichukuliwa na Aziz Andambwile, Ben Starkie na George Mpole ili kuongeza nguvu kwenye eneo la kiungo na ushambuliaji.

Mabadiliko hayo yalionyesha kuinufaisha zaidi Stars ambayo ilishambulia kwa kasi mara kwa mara ili kusawazisha bao hilo.

Dakika ya 71, Simon Msuva aliipatia Stars bao la kusawazisha baada ya kupiga mpira uliomshinda kipa, Mustafa Mohamed kufuatia mabeki wa Sudan kudhani nyota huyo kaotea.

Baada ya bao hilo Stars iliendelea kufanya mabadiliko kwa kumtoa Mbwana Samatta huku nafasi yake ikichukuliwa na Reliants Lusajo.

Kwa upande wa Sudan alitoka kiungo, Safour Walieldin na kuingia Gazafe Mohamed kwa ajili ya kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji.

Stars Ilifanya mabadiliko dakika ya 80, kwa kumtoa Nickson Kibabage huku nafasi yake ikichukuliwa na Farid Mussa ambapo hata hivyo mabadiliko hayo hayakuleta matokeo chanya.

Hii ni mechi ya pili kwa Stars baada ya awali kuibuka na ushindi wa mabao 3-1, dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, mchezo uliopigwa Machi 23.

Mechi hii iliyo kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) ni maandalizi kwa Stars inayojipanga na michezo ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) itakayofanyika kuanzia Januari 8-31, 2023 nchini Algeria.

Mbali na CHAN Lakini pia na fainali za mataifa ya Afrika (AFCON), itakayofanyika kuanzia Juni 23 hadi Julai 23, 2023 nchini Ivory Coast.