Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msolla aunda Kamati ya ujenzi

Muktasari:

Wengine ni Arch. Joseph Peater, Hamad Islam, Qs. Suma Mwaitenda, Ashura Ande, James Lobikoki, Qs. Gervas Kondobole, Injinia Isaac Chanji, Injinia Madaraka Marumba, Rena Calist na Dk Abdallah Mrindoko.

MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msola ameteua wajumbe 20 kwaajili ya kuunda kamati ya ujenzi na miundombinu ya klabu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano, imeeleza kuwa kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti, Injinia Bahati Mwaseba akisaidiana na Makamu wake Dk Athuman Kihamia na Katibu akiwa ni Said Mrisho.

Wajumbe wengine walioteuliwa ni Mbaraka Igangula, Said Hersi, Fundi Sayole, Buluba Mabelele, Heriel Muhulo, Isack Usaka,  Jumanne Warema ambao wote ni mainjinia.

Wengine ni Arch. Joseph Peater, Hamad Islam, Qs. Suma Mwaitenda, Ashura Ande, James Lobikoki, Qs. Gervas Kondobole, Injinia Isaac Chanji, Injinia Madaraka Marumba, Rena Calist na Dk Abdallah Mrindoko.

Katika hatua nyingine Kamati ya Utendaji imemuongeza Ester Cheyo kuwa mjumbe kwenye kamati ya Sheria na Nidhamu, kumtaja John Mwangata kuwa mjumbe wa kamati ya hamasa na habari ambaye awali jina lake lilisomeka Patrick Mwangata.