Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msiba wa Ruge Mutahaba waibua kali tano, Jeneza lake litapita njia hizi

Muktasari:

Watanzania baada ya kupata taarifa ya msiba  wa Ruge Mutahaba,siku hiyo hiyo na siku zinazoendelea kuusubiri mwili wa Ruge, wasanii wa fani tofauti wameingia studio kurekodi wimbo wa maombelezo wa kifo cha Ruge Mutahaba

Dar es Salaam.Tangu kutokee msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba Feb 26,2019, kumekuwepo na matukio mbalimbali yanayoendelea kujitokeza huku ukisubiriwa mwili wake kuingia leo Ijumaa kutoka Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu.
Awakutanisha Steve Nyerere na Ommy Dimpoz
Ruge ameweza kuwakutanisha wasanii wawili wanaodaiwa kuwa na bifu, nao ni Steve Nyerere  na Ommy Dimpoz.
Katika msiba huo uliopo nyumbani kwa wazazi wa Ruge Mutahaba Mikocheni jijini Dar es Salaam, alianza kufika Steve Nyerere  na baada ya muda akafika Ommy Dimpoz  na kwenda moja kwa moja kwenye kibaraza kusalimia ndugu na watu waliokuwa wamekaa,akatoka na kwenda kukaa kwenye viti vya mbele.
Steve Nyerere alimfata Ommy Dimpoz sehemu aliyokaa kwenda kumsalimia,walikumbatiana kwa furaha, huku Steve Nyerere akimtamkia  Ommy amsamehe kuwa ni mdogo wake hivyo ni ndugu yake basi wasamehane.
"Ebwanaa Ommy uko poa,wewe ni ndugu yangu ,mdogo wangu,hivyo tusamehane kwa yaliyotokea,maana leo ndio kwa mara ya kwanza nakuona toka uingie nchi baada ya kupona" alisikika Steve Nyerere akiongea hapo msibani kwa Ruge
Kwa upande wa Ommy Dimpozi yeye alisema Steve Nyerere ni kaka yake hawajajuana leo,yaliyopita sio ndwere wagange yajayo kwani binadamu hawajakamilika,ila kikubwa zaidi  ni kuishi kwa upendo.
"Mimi bwana, Steve Nyerere ni kaka yangu,na hatujajuana leo wala jana, hivyo yaliyopita sio ndwere tugange yajayo, kwani kila binadamu anamapungufu yake hakuna mkamilifu,kikubwa ni kuishi kwa furaha na upendo kama hivi unavyotuona na Steve tumefika tumekumbatiana," alisikika kiongea Ommy Dimpoz
Baada ya kuombana msamaha hiyo Steve Nyerere na Ommy Dimpoz walianza kutaniana, ambapo Ommy Dimpoz alimuuliza Steve Nyerere Vocal yake inatokea wapi, steve akamuonyesha kooni wakacheka, Steve nae akamwambia Ommy Dimpoz kesho yake atakuwa na vikao ubalozini na viongozi wa nchi na baada ya hapo ataonana na Makonda hivyo wataonana jioni na Dimpoz, wakacheka Ommy Dimpoz akamuuliza hautakuwa na kikako cha kamati ya mazishi?wakaendelea kucheka.

Wasanii watunga wimbo wa maombolezo.
Watanzania baada ya kupata taarifa ya msiba  wa Ruge Mutahaba,siku hiyo hiyo na siku zinazoendelea kuusubiri mwili wa Ruge, wasanii wa fani tofauti wameingia studio kurekodi wimbo wa maombelezo wa kifo cha Ruge Mutahaba.
Wasanii hao ambao kila fani wamerekodi  studio tofauti tofauti ,ambapo wasanii walioanza darasa mwanzo THT, kama Lina, Mwasiti, Barnaba, Amin, Dogo Ditto, Beka, Ally Nipishe wametunga wimbo unaoitwa "Asante Baba" wamerekodi katika Studio ya Barnaba iloyopo Kinondoni.
Na wapo ambao wanaoendelea na Darasa THT kama Jay Melody na wenzake nao wameingia studio kutoa wimbo wa maombolezo kifo cha Ruge.
Kwa upande wa wanamuziki wa Dansi ,nao hawakuwa nyuma wametunga wimbo wa maombelezo unaoitwa "Kwaheri Ruge Mutahaba" na kurekodiwa studio ya Elasto Mashine iliyopo Kinondoni jijini Dar es Saalam.
Wanamuziki hao ambao ni wa bendi tofauti tofauti ni Kalala Junior, Haji Makuke 'Haji BSS' Jimmy Manzaka, Khali Chokoraa, Chaz Baba, Nyoshi El Saadat, Jose Mara, Isha Mashauzi, Abdull Misambano
Wapiga vyombo wa wimbo huo wa dansi ni Christian Mene, Kapiga magitaa yote,Kaposhoo Tumba,kapiga Tumba,Erasto Mashine kapiga Kinanda na kuprogram biti maana yeye ndio production.

Jamani achene visasi
Siku ya pili ya msiba wa Ruge, Feb 27,2019 msanii wa filamu Jacline Wolper alitinga msibani,baada ya salamu kwa ndugu wa marehemu,waandishi wa habari walimfata na kumuhoji maswali.
Kabla hajaanza kujibu maswali ya waandishi, Wolper alianza kuongea haya: "Kwanza napenda kutoa ushauri kwa wasanii wenzangu wa fani zote,na hata wasiokuwa wasanii, yaani watu wakawaida,tuepuke kuishi kwa visasi hata kama tumeumbwa na hasira na kushindwa kuzizuia,hivyo tujaribu kuangalia mbele,maana kitu kinaweza kisikukute wewe ila kuna vizazi unaviacha  au vinavyokuja ukaviumiza.
"Sababu huwezi jua Ruge amemsaidia nini  mtu au watu , hivyo unavyoonyesha chuki zako mbele za watu  au mtu ,na yule mtu au watu wakaona  kama hawezi kukutendea wewe baya basi anaweza kutendea kizazi chako,hivyo watu waache mambo ya visasi na kujiona maisha wameshayapatia wakati kunavizazi vyake vipo vitateseka kama kuna mtu anahasira na
marehemu Ruge,azizuie hasira zake kwa kunywa maji,ila ajiangalie mara mbili mtu hajafa unakuwa nae na hasira na amefariki bado unaendekea kuwa na hasira hii sio nzuri"
Pia Wolper alimpongeza Mwakyembe kwa kitendo cha kutoa kauli ya kukamatwa kwa msanii Dudubaya kwa kosa la kumdhihaki Ruge.
Hata hivyo, Wolper anasema hana cha kumshauri msanii Diamond kwa  kushindwa kutoa ushirikiano wakati Ruge anaumwa na hata kutomposti katika mitandao, kwani hajui walichofanyia na Ruge na ukiangalia Diamond ni mtu mzima anaelewa zuri na baya.

Kaka wa Diamond atinga msibani
Kitendo cha kaka wa Diamond,Romy Jones kutinga msibani baada ya taarifa ya msiba wa Ruge jioni tu ulipotokea, kitendo hicho kiliwashangaza watu haswa wanaodai kuwa kampuni ya wasafi na Ruge wana bifu.
Romy Jones alizungumza na Mwanaspoti na kusema kuwa, yeye amekuwa mtu wa kwanza kufika kwenye msiba wa Ruge, sababu mwanamke aliyemuoa amezaa na Ruge mtoto mmoja na hata hivyo, Ruge ni mtu muhimu sana kwake na ndiye aliyemtoa kwani alishawahi kufanya kazi naye.
"Mimi huu msiba unanihusu sana tu,kwanza mimi mwanamke niliyemuoa amezaa na Ruge mtoto mmoja kabla ya mimi kumuoa,na pia mimi Ruge nimeshawahi kufanya nae kazi na ndiye aliyenitoa na kujulikana" alisema Romy

Wasikie wafanyakazi Clouds
Katika kuendelea kuusubiri mwili wa Ruge Mutahaba,wafanyakazi baadhi wa Clouds, walitawaliwa msibani kwa kumbukumbu ya kauli ya Ruge Mutahaba kuwa akifa "wasilie wafurahie'
Wafanyakazi hao walipiga stori na Mwanaspoti na kusema Ruge alipokuwa anaumwa, alitoa kauli hiyo kwa wafanyakazi wake kuwa ilitokea amefariki, basi wasilie ila washeherekee.
"Kauli ni moja tu jamani, tusijisahau bosi alivyotuambia  wakati akiwa anaumwa siku akifa, wafanyakazi tusilie ila tusheherekee."