Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mshambuliaji wa Stand asajiliwa timu ya Ligi Kuu Zimbabwe

Muktasari:

Chidiebele amesaini mkataba huo kwa uhamisho huru baada ya mkataba wake na Stand kumalizika.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Stand United, Abasilim Chidiebele amesaini mkataba wa miaka miwili leo Jumatano kuichezea timu ya Caps United inayoshiriki Ligi Kuu nchini Zimbabwe.

Chidiebele amesaini mkataba huo kwa uhamisho huru baada ya mkataba wake na Stand kumalizika.

Mshambuliaji huyo alisema kuwa usajili wake ulikuwa ufanyike mapema lakini ulichelewa kutokana na kushindwa kufikia makubaliano ya maslahi binafsi ambayo hatimaye wamefikia muafaka baina yake na timu hiyo.

"Napenda kutumia fursa hii kumshukuru Mungu, familia yangu, Stand United na mashabiki wote wa soka Tanzania kwa kuishi vizuri na mimi katika kipindi chote nilichocheza ligi ya hapo, " alisema mshambuliaji huyo.