Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKT Queens yaivua Simba Queens ubingwa WPL

Muktasari:


  • Ushindi huo umeifanya JKT Queens kumaliza msimu na pointi 47 sawa na Simba Queens lakini zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

JKT Queens imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Soka Wanawake (WPL) msimu huu wa 2024/2025 baada ya leo Mei 20,2025 kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Gets Program.

Ushindi huo umeifanya JKT Queens kumaliza msimu na pointi 47 sawa na Simba Queens lakini zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

Katika mchezo huo, JKT Queens dakika 35 za mwanzo zilishaonyesha kuwa ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa baada ya kuwa mbele kwa mabao 3-0 yaliyowekwa kimiani na Anastanzia Katunzi dakika ya sita, Stumai Abdallah dakika ya 24 na Wilfred Gerard dakika ya 31 ambaye alifunga lingine dakika ya 68, huku la mwisho likipachikwa na Janet Matulanga dakika ya 87.

Simba Queens ambayo nayo ilikuwa na nafasi ya kuchukua ubingwa huo, imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Alliance Girls. Mabao ya Simba Queens yaliwekwa kimiani na Jentrix Shikangwa na Shelda Boniface.

Huu ni ubingwa wa nne kwa JKT Queens baada ya kuutwaa msimu wa 2017/2018, 2018/2019 na 2022/2023, ikiwa sasa imemaliza kiburi cha Simba Queens ambayo ilikuwa ndiyo timu ilitwaa ubingwa huu mara nyingi (4), msimu wa 2019/2020, 2020/2021, 2021/2022 na 2023/2024.

Stumai Abdallah wa JKT Queens, ameibuka mfungaji bora wa ligi hiyo baada ya kufunga mabao 28.

Matokeo mengine yameshuhudia Yanga Princess ambayo imemaliza nafasi ya tatu ikiambulia sare ya mabao 2-2 dhidi ya Ceasia Queens, Mashujaa Queens ikiichapa Bunda Queens 3-1 na Fountain Gate Princess ikiipa dozi nzito Mlandizi Queens ya mabao 6-0.

Baada ya kumalizika kwa msimu huu, timu kongwe kwenye soka la Wanawake, Mlandizi Queens imeshuka daraja ikiwa na pointi moja sambamba na Gets Program iliyomaliza na pointi 10.


ORODHA YA MABINGWA LIGI YA WANAWAKE
2017: Mlandizi Queens
2017/2018: JKT Queens
2018/2019: JKT Queens
2019/2020: Simba Queens
2020/2021: Simba Queens
2021/2022: Simba Queens 
2022/2023: JKT Queens
2023/2024: Simba Queens
2024/2025: JKT Queens