Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mrundi mpya aanza na mikwara Simba, Mosoti akubali yaishe

Beki wa timu ya Simba Donald Mosoti akifanya mazoezi chini ya kocha wake Patrick Phiri.Picha na Doris Maliyaga

Muktasari:

Phiri amekiri kwamba beki huyo, Hussein Butoyi ameanza vizuri lakini hata Mosoti amekuwa akifanya vizuri mazoezini katika muda wote ndiyo maana anahitaji kumtathmini zaidi na kuangalia viwango vya wachezaji hao wawili kwa kina.

BEKI Mrundi aliyeshushwa Msimbazi kufanya majaribio, ameanza mazoezi jana Alhamisi mjini hapa kwa mikwara ya aina yake ambayo imemfanya kocha Patrick Phiri kumwangalia mara mbilimbili na kutikisa kichwa ingawa ametamka kwamba hatafanya uamuzi kwa kukurupuka.

Phiri amekiri kwamba beki huyo, Hussein Butoyi ameanza vizuri lakini hata Mosoti amekuwa akifanya vizuri mazoezini katika muda wote ndiyo maana anahitaji kumtathmini zaidi na kuangalia viwango vya wachezaji hao wawili kwa kina.

“Nimemuona katika mazoezi haya, Mosoti ni beki mzuri hata huyu mpya (Hussein) pia ni mzuri ila nitaendelea kumwangalia zaidi. Nahitaji muda kabla ya kufanya uamuzi wowote,” alisema Phiri ambaye ni mpole, lakini anayependa soka la kuvutia uwanjani.

Butoyi ambaye Simba walimuona kwenye michuano ya Kagame akiichezea Telecom ya Djibouti, alifanya mazoezi kwa nguvu juzi Jumatano jioni na jana asubuhi akijitahidi kuonyesha ubora wake na kujenga imani kwa Phiri.

Mchezaji huyo alionyesha urafiki na wachezaji kadhaa wa Simba ndani na nje ya uwanja.

Kamati ya Usajili ya Simba imemtanguliza Butoyi ili afanye majaribio na Simba na kama Phiri akimkubali, basi atachukua nafasi ya Mkenya Donald Mosoti ambaye anataka kuachwa kwa vile amepata timu Qatar.

Endapo Phiri hataridhika na uwezo wa mchezaji huyo, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zacharia Hanspoppe, aliyeko Rwanda kwenye Kombe la Kagame atamleta beki mwingine wa APR.

Mosoti akubali yaishe

Mosoti amesema kwamba hata ikitokea anapata nafasi ya kuondoka katika kikosi cha Simba kabla ya Desemba kama walivyokubaliana, haitakuwa tatizo kwani ni mpango ambao upo ingawa alipendelea kuachana na timu hiyo wakati wa dirisha dogo la usajili.

Awali, Mosoti aliomba kuvunja mkataba na Simba ili akajiunge na timu moja nchini Qatar ambayo alikwenda kufanya majaribio na kufuzu, hata hivyo ilishindikana kuondoka kutokana na kuwa na mkataba mrefu na Simba.

“Nilizungumza na viongozi wangu wa Simba kuhusu hilo, walinikubalia kuwa nikitaka kuondoka nitaruhusiwa, baada ya mazungumzo niliona ni vyema niondoke Desemba ila kulikuwepo na makubaliano kwamba ikitokea hata kabla ya Desemba niruhusiwe hivyo hakuna tatizo kwa hilo,” alisema Mosoti.

Phiri aanza kujipima

Kocha Phiri amesema anaanza kukipima kikosi chake kwa mechi ndogo ndogo kabla ya kucheza na timu kubwa pamoja na mechi za kimataifa.

Simba ipo visiwani hapa inafanya mazoezi yake kwenye uwanja wa Chuoni Chukwani. Keshokutwa Jumapili usiku itacheza mechi yake ya kwanza ya kirafiki na timu ya daraja la pili ya Kilimani City, mechi hiyo itafanyika Uwanja wa Amani na kufuatiwa na nyingine kadhaa.