Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mrembo aliyevamia fainali sasa maarufu

Muktasari:

Kutokana na kitendo chake cha kuingia uwanjani huku umbo lake likiwa na mvuto kwa watazamaji, akaunti ya Instagram ya Kinsley iliyokuwa na mashabiki 230, 000 iliongezeka wafuasi kufikia zaidi ya milioni mbili. Wengi walipenda kumjua zaidi.

MADRID, HISPANIA.GHAFLA amekuwa maarufu duniani kote! Hatimaye mrembo aliyeingia uwanjani nusu uchi katika pambano la fainali ya Ulaya kati ya Liverpool na Tottenham Uwanja wa Wanda Metropolitano amefahamika kuwa ni Kinsey Wolanski kutoka Russia.

Kinsey alisimamisha kwa muda pambano hilo baada ya kuingia uwanjani akiwatoroka walinzi wa uwanja ambao huwa wanajipanga vyema kwa ajili ya kudhibiti mashabiki wanaoweza kuingia uwanjani. Kamera ilimnasa kwa sekunde kadhaa kabla ya kugeukia wachezaji wengine.

Kinsey amefahamika ni mrembo ambaye anafanya masuala yake katika mtandao wa Instagram na aliingia uwanjani na nguo ya kuogelea ambayo ilikuwa imeandikwa jina la Vitaly Uncensored akitangaza mtandao wa Youtube wa Boyfriend wake, Vitaly Zdorovetskiy ambaye ni maarufu kwa kumiliki akaunti ya Mtandao wa Youtube iitwayo Vitalytv.

Kutokana na kitendo chake cha kuingia uwanjani huku umbo lake likiwa na mvuto kwa watazamaji, akaunti ya Instagram ya Kinsley iliyokuwa na mashabiki 230, 000 iliongezeka wafuasi kufikia zaidi ya milioni mbili. Wengi walipenda kumjua zaidi.

Baadaye aliandika katika mtandao wake wa Youtube akidai ‘Kuvamia uwanja wa Ligi ya Mabingwa, maisha yapo kwa ajili ya kuishi, kufanya vitu vya kiwehu ambavyo utavikumbuka kwa maisha yako yote.”

Wolanski anadai alishikiliwa na polisi kwa saa tano kabla ya kuachiwa lakini kabla ya hapo walihakikisha kwa muda wote aliokuwa katika kituo chao alikuwa amejifunika mwili wake vyema tofauti na awali.

“Walinipeleka katika kituo cha polisi na kuniweka ndani kwa saa tano kabla ya kuniruhusu niondoke. Nikiwa uwanjani palepale walinipa kivazi kama cha hospitali kwa ajili ya kufunika mwili wangu, kwa hiyo kama vile nilikuwa jela nikiwa na nguo za hospitali.”

Mara baada ya kutoka ndani huku mtandao wake wa Instragram ukizidi kupata wafuasi wengi baadaye mtandao huo ulitoweka hewani kwa kile kinachodaiwa ofisi za Instagram zilikuwa zimeamua kuufunga lakini mwenyewe alidai wadukuzi wa mitandaoni walikuwa wameuchukua.

Wolanski baadaye alitania kutokana na jinsi umbo lake lilivyokuwa, sio mashabiki tu waliokuwa wanatazama katika televisheni ndio walivutiwa naye bali hata kiungo wa Tottenham, Harry Wink ambaye alikuwa karibu naye pia alivutiwa na umbo lake.

Wolanski pia alidai alikuwa peke yake na wapenzi wa Liverpool wakati akifikiria namna ya kuvamia uwanjani lakini kamera nyingine ilionyesha alikuwa amekaa na mpenzi wake, Zdorovetskiy. “Nilikuwa uwanjani peke yangu. Nilimuuliza mtu ambaye alikaa karibu yangu kama anaweza kunishikia simu yangu na nikakimbilia uwanjani.”

Kutokana na mashabiki wengi kuanza kumfuatilia katika akaunti yake ya Instagram mara baada ya tukio hilo, Wolanski aliwashukuru mashabiki wake hao wapya katika mtandao wa Instagram akidai: “Jamani hamuwezi hata kujua hisia nilizonazo kwa sasa, najisikia vizuri sana na nashukuru, natamani kulia.

“Nilifanya hivyo kwa sababu nilitaka niachane na maisha yangu ya kila siku ya kawaida. Napenda hisia hizo. Najisikia vyema kufanya vitu vya ajabu. Napenda kufanya vitu vya ajabu muda wote, lakini siamini kama ingefikia hatua hiyo, asanteni wote kwa meseji za kunisapoti na kunishukuru. Kila kitu kimekwenda sawa.”

Umaarufu wa Wolanski katika dunia ya masuala ya mitindo ulianza wakati alipoonekana akiwa safarini kwenda Los Angeles Marekani. Tangu hapo ametokea katika majarida mbalimbali kama vile Sports Illustrated, FHM na Maxim.

Kwa upande wa mpenzi wake, Zdorovetskiy ambaye ni Mrusi aliyechenganya na Mmarekani yeye ni maarufu zaidi katika mitandao wa Yotube akiwa na Chaneli yake ya VitalyzdTv ambayo mpaka sasa video yake imetazamwa na watu 1.65 bilioni huku watu waliojiandikisha kwake wakiwa ni 9.9 milioni.

Mara baada ya mpenzi wake kufanya alichofanya katika mtandao wa Youtube, Zdorovetskiy alifurahishwa na alichokiona huku akiandika katika mtandao wa Instagram: “Mpenzi wangu kipenzi ameingilia fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, najivunia, wewe ni kila kitu kwangu.”

Wakati ukishangazwa na Wolanski kumbe hata bwana wake, Zdorovetskiy naye aliwahi kupata jina kwa kufanya kitendo kama hicho. Mwaka 2014 katika pambano la fainali Kombe la Dunia kati ya Ujerumani na Argentina aliingia uwanjani na kuvuruga mechi kwa muda.

Awali Zdorovetskiy alijaribu kumkumbatia beki wa Ujerumani, Benedikt Howedes lakini akaondolewa na walinzi. Zdorovetskiy pia aliwahi kuingia uwanjani katika pambano la fainali za baseball mwaka 2017 lakini akawahiwa.

Tayari Zdorovetskiy amedai anataka kumuoa Wolanski na alikuwepo nje ya kituo cha polisi wakati mrembo wake alipoachiwa huku akimpiga vibao katika makalio kwa furaha baada ya jaribio lake la kuingia uwanjani kufanikiwa.

Wawili hao wanaonekana kuwa katika penzi zito kwa sasa na picha zao za Instagram ambazo nyingi zinawaonyesha wakiwa katika mahaba mazito huku viwalo vyao vikiwa vya wazi zaidi. Hivi karibuni Vitaly aliposti picha akimbusu Wolinski huku akimshukuru kwa kutembea naye duniani kote.

“Asante kwa kusafiri na mimi, Uturuki-Iceland- Israel- Uholanzi Italia- UAE-Ufaransa-Mexico-Ugiriki- Afrika Kusini-Hispania-Ubelgiji na nchi kibao. Asante sana haitoshi, niseme nakupenda sana,” aliandika Vital katika mtandao wake wa Instagram.