Morrison ndio basi tena Simba

Friday May 13 2022
Morrison PIC
By Thobias Sebastian

KLABU ya Simba imempa mapumziko hadi mwisho wa msimu mchezaji wake, Bernard Morrison kutokana na sababu ambazo hawakuziweka wazi.

Simba imefikia maamuzi hayo baada ya pande zote mbili kukubaliana kwa lengo la kumpa nafasi Morrison kupumzika na kushuhulikia mambo yake binafsi.

Simba inamshukuru Morrison kwa mchango wake kwa kipindi chote alichohudumia ndani ya klabu yao.

"Tunatambua na kuthamini mchango wa Morrison katika miaka miwili aliyotumikia klabu yetu na kuisaidia kupata mafanikio kadhaa kucheza robo fainali ya michuano ya Afrika mara mbili," ilieleza taarifa hiyo;

Morrison1

"Kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Ubingwa wa kombe la Shirikisho (ASFC) na ubingwa wa kombe la Mapinduzi,

Advertisement

"Kwa mchango na mafanikio hayo klabu inamshukuru mchezaji huyo kipenzi cha Wanasimba kwa kujitoa kwake kuipigania klabu yake.

"Simba inamtakia kila la heri Morrison katika mapumziko yake na safari yake ya soka hapo baadae."

Advertisement