Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Moallin, Maxi wakoleza paredi la Yanga

Muktasari:

  • Yanga inafanya paredi hilo baada ya kutwaa ubingwa wa tano mfululizo na wa 32 kiujumla wa Ligi Kuu Bara tangu mwaka 1965.

KAIMU kocha Mkuu wa Yanga, Abdihamid Moallin na mchezaji Maxi Nzengeli wamekoleza paredi la ubingwa la kikosi hicho linalofanyika leo Jumamosi Julai 4, 2026, lililoanzia mitaa ya Karume jijini Dar es Salaam.

Yanga inafanya paredi hilo baada ya kutwaa ubingwa wa tano mfululizo na wa 32 kiujumla wa Ligi Kuu Bara tangu mwaka 1965.

Katika shamrashamra hizo zinazoendelea, Moallin aliyeipa taji timu hiyo ameonekana akiwa mwenye furaha sambamba na nyota wengine wakiongozwa na Maxi Mpia Nzengeli.

Moallin na Maxi wamepanda gari maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya shamrashamra hizo, sambamba na mastaa wengine, wakiwemo, Mohamed Damaro na Kouassi Attohoula Yao.

Wachezaji hao na benchi la ufundi la Yanga likiongozwa na Moallin liko kwenye gari maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya paredi hilo, lililoanza saa 7:00 mchana katika mitaa ya Karume jijini Dar es Salaam zilipo Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).