Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mnigeria Simba aomba radhi kisa Yanga

Mnigeria Simba aomba radhi kisa Yanga

WINGA mpya wa Simba, Nelson Okwa amesema bado haamini kama timu hiyo imepoteza mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, kisha akaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo na kuahidi kwenda kujipanga upya kwa mechi za Ligi Kuu Bara na michuano mingine ili wafanye vizuri zaidi.

Okwa aliyesajiliwa hivi karibuni kutoka Rivers United ya Nigeria na kuingizwa kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Kibu Denis, alisema matokeo hayo yamewaumiza mno, lakini kwa vile soka ndivyo lilivyo na mshindi ilikuwa lazima apatikane wanaenda kujipanga upya kwa ajili ya Ligi.

Okwa alisema anafahamu Simba ilipewa nafasi kubwa ya kupata ushindi, hata hivyo baada ya matokeo hayo si vyema kuangalia tena nyuma bali kuweka nguvu katika michezo ijayo.

Alisema makosa yaliyotokea hadi kupoteza wanakwenda kuyafanyia kazi katika mazoezi chini ya benchi lao la ufundi ili wakirejea tena katika mchezo wa kimashindano kupata matokeo tofauti na hayo.

“Kweli tulikuwa vizuri kipindi cha kwanza ila mpira ndivyo ulivyo, si jambo zuri kwetu kama wachezaji ila limetuuma na tunakwenda kulifanyia kazi ili kuhakikisha furaha inarejea,” alisema Okwa ambaye shuti lake liligonga nguzo Yanga na kuongeza;

“Tutarudi kwa nguvu katika mashindano mengine yaliyo mbele yetu kwani si vyema kuongeza zaidi wakati huu bali tunatakiwa kufanya kazi uwanjani.”