Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mnahesabu lakini? Mara ya tatu mjue

Muktasari:

Kiiza jana alifunga mabao mawili na kufikisha mabao 18, moja zaidi ya Tambwe aliyempiku juzi Jumanne wakati Yanga ikiisulubu Africans Sports kwa mabao 5-0.

MWENDO mdundo. Simba jana Alhamisi kwa mara ya tatu imekalia kiti cha uongozi wa Ligi Kuu Bara baada ya kuicharaza Ndanda FC ya Mtwara mabao 3-0, huku Hamis Kiiza akimmzidi ujanja Amissi Tambwe wa Yanga katika mbio za ufungaji bora.

Kiiza jana alifunga mabao mawili na kufikisha mabao 18, moja zaidi ya Tambwe aliyempiku juzi Jumanne wakati Yanga ikiisulubu Africans Sports kwa mabao 5-0.

Mganda huyo alifunga mabao hayo katika kipindi cha pili baada ya awali kiungo Mwinyi Kazimoto kutangulia kuiandikia Simba bao dakika ya 36.

Kiiza alifunga bao lake la kwanza lililokuwa la pili katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam dakika ya 57 akiunganisha mpira wa kona wa Ibrahim Ajib kabla ya kuongeza jingine dakika ya 72 akimalizia pasi ya Danny Lyanga.

Ndanda licha ya kujitahidi kutaka kurejesha mabao hayo, juhudi zao ziliishia kwa mabeki wa Simba waliongoza na Novaty Lufunga na Juuko Murshid.

Mjini Mbeya, wenyeji Mbeya City waliitandika Stand United kwa mabao 2-0 katika mchezo mwingine mkali wa Ligi Kuu Bara. Mabao ya washindi yalitumbukizwa wavuni dakika ya 13 na Raphael Alfa aliyeuwahi mpira wa penalti aliyopiga awali uliotemwa na kipa wa Stand kabla ya Haruna Shamte kuongeza la pili wa mpira wa adhabu ndogo nje ya 18 katika dakika ya 47.

Simba: Vincent Angban, Hassan Kessy, Mohammed Hussein, Novart Lufunga, Murshid Juuko, Justice Majabvi, Mwinyi Kazimoto/Mussa Mgosi, Jonas Mkude, Hamis Kiiza, Ibrahim Ajib/Danny Lyanga na Said Ndemla/Awadh Juma.

Ndanda: Jeremia Kisubi, Azizi Sibo, Paul Ngalema, Kassim Ponela, Salvatory Ntebe, Hemed Khoja, William Lucian, Omega Seme/Bryson Raphael, Omary Mponda/ Salum Mineli, Atupele Green na Kiggy Makassy/ Hamad Msumi.

Imeandikwa na Olipa Assa, Dar na Godfey Kahango, Mbeya.

Wakati huo huo uongozi wa Simba umesema umepokea kwa masikitiko taarifa za kuugua kwa kipa wao wa zamani Abel Dhaira aliyegundulika kuugua kansa ya utumbo, ikidai wapo pamaja na mchezaji huyo na familia katika kipindi hiki kigumu.