Mmoja afariki Dunia kwa Mkapa

Muktasari:
- Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa afya Ummy Mwalimu kupitia akaunti yake mtandao wa Twitter ametoa taarifa ya hali iliyotokea Uwanja wa Mkapa baada ya mashabiki kusongamana nje ya mageti na mengine kuvunjwa na mashabiki kuingia kwa nguvu uwanjani na hadi sasa majeruhi ni 30 huku mtu mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka 40 amefariki dunia.
Leo katika Uwanja wa Benjamini Mkapa Yanga ikicheza fainali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger, wakati msongamano wa mashabiki wakiingia uwanjanni muda mchache kabla ya mechi umesababaisha kifo cha mtu mmoja na wengine wajeruhiwa.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa afya Ummy Mwalimu kupitia akaunti yake mtandao wa Twitter ametoa taarifa ya hali iliyotokea Uwanja wa Mkapa baada ya mashabiki kusongamana nje ya mageti na mengine kuvunjwa na mashabiki kuingia kwa nguvu uwanjani na hadi sasa majeruhi ni 30 huku mtu mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka 40 amefariki dunia.
"Timu ya wataalam wa Huduma za Dharura ya Hospitali ya Taifa Muhimbili imeshawasiliana na Hospitali ya Rufaa Ya Mkoa Temeke na wapo standby kupokea na kuwahudumia majeruhi ambao watahitaji matibabu zaidi," ameeleza Waziri Ummy
Msongamano wa mashabiki kuingia uwanjani ulikuwa mkubwa na kila ambapo watu wa usalama walipokuwa wakiwazuia geti moja walikimbilia lingine na kuingia.